User:Robert Ullmann/Mwananchi/1 January 2009

User:Robert Ullmann/Mwananchi/header

adhabu
Hakimu huyo, baada ya kuridhika na ushahidi, alitoa adhabu hiyo ya miaka mitatu jela kwa kila kosa ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaofanya makosa kama hayo. [1]
aina
FUVU la kichwa cha binadamu limekutwa nyumbani kwa mfanya biashara maarufu wa Maili moja mjini Kibaha, Ally Msuya maarufu kwa jina la Puku likiwa limehifadhiwa kwenye ndoo ndogo aina ya Sadolini iliyokuwa na mafuta ya kupikia yanayojulikana kwa jina la samli. [2]
ajili
Tena tulikuwa tunafanya hivyo kwa ajili ya kuendeleza manufaa binafsi ya kisiasa. [3]
akisema
Mwenyekiti huyo pia alisema kuwa Halmashauri ya Kuu ya CCM mkoani Mbeya inakanusha chama hicho kimegawanyika, akisema kuwa, hakuna wabunge waliogawanyika ndani ya chama hicho. [4]
ama
Katibu wa matajiri hao wa mafuta nchini, Bisarara alisema akiba yao inatosha na kwamba hakuna haja ya wananchi ama serikali kuwa na wasiwasi kwamba bidhaa hiyo inaweza kupungua. [5]
ambaye
Kaimu kamanda wa polisi, Kilongo tukio hilo lilitokea Desemba 30, 2008 na kumtaja aliyeuawa kuwa ni Mwandu Mayala, 40, mkazi wa kijiji cha Ihalo ambaye anadaiwa kuiba mpunga huo mali ya Zakaria Shija. [6]
ana
Akijitetea kabla ya hukumu hiyo, Kulyama alidai apunguziwe adhabu kwa sababu ana familia inayomtegemea na wazazi na kwamba tayari ameshapoteza kazi, lakini utetezi wake ulitupiliwa mbali na hakimu huyo. [7]
askari
Katika mkutano huo pia walikuwapo maafisa usalama wa taifa na makachero waliokuwa wakisaidiana na askari wa Jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa wafuasi wa Chadema hawafanyi vurugu. [8]
bado
Baada ya kuangalia kumbukumbu za mahakama Hakimu Kabate alimweleza Rama kuwa upelelezi bado haujakamilika na kumtaka aulize swali lingine. [9]
bali
Kimsingi siungi mkono si tu kwa sababu Mkapa ni wa kusini bali alivyoliongoza taifa," alisema Athumani akimzungumzia Mkapa ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Lupaso wilayani Masasi. [10]
bei
Basi mheshimiwa hakimu naomba hela nikanunue soda maana kila siku nasikia soda zimepanda bei lakini mimi sijawahi kunywa,"alisema Rama. [11]
cha
Tumeunda kikosi-kazi kinachojumuisha Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa cha kuendesha mapambano haya," alisema Kikwete. [12]
chake
Alisema mauaji hayo ni ya mateso na hayana sababu ya kwa kuwa chanzo chake ni cha kipuuzi na kwamba wanaoamini kuwa wakipata viungo vya albino watatajirika, waganga na wauaji serikali itawabana. [13]
chama
Lakini jana mgombea huyo na chama chake waliendelea na kampeni kana kwamba hajaenguliwa na kuonekana kuwa na uhakika wa kuwemo kwenye kinyang'anyiro hicho. [14]
dola
Wakati bei ya mafuta ikipanda nchini, hali ni tofauti katika soko la dunia ambako nishati hiyo imeshuka kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita baada ya kupanda kwa kasi hadi kufikia dola 140 za Kimarekani kwa pipa mwezi Julai. [15]
dunia
Lakini, hali ingekuwa bora zaidi kama uchumi wa dunia usingepata misukosuko. [16]
elimu
Mkurugenzi wa vijana wa Chadema, John Mnyika ndiye aliyekuwa wa kwanza kuusisimua umati huo, baada ya kuwataka wananchi hao kumuuliza mgombea wa ubunge wa CCM, Mchungaji Luckson Mwanjali, kiwango chake cha elimu na kuwa ana uwezo gani wa kuwasaidia. [17]
endapo
Mwenyekiti wa CCM mkoani Mbeya, Nawabu Mulla alitoa onyo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari kuwa wabunge wa CCM wagawanyika na kuwa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi atakashifiwa endapo atahudhuria uzinduzi huo. [18]
es
Wakati fulani wanafunzi wa sekondari waliandamana hadi ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, wakirusha maneno makali dhidi ya serikali, wakidiriki kuiita kuwa ni ya kisanii. [19]
fuvu
Kwa mujibu wa mashuhuda na majirani walisema kuwa fuvu hilo ambalo lilikuwa limehifadhiwa kwenye kisadolini kidogo lilikuwa limehifadhiwa ndani ya mafuta aina ya Samli ili lisiweze kutoa harufu kali ya uozo ndani ya nyumba hiyo kwa kipindi chote ambacho ililengwa kikae humo. [20]
hali
Akizungumzia hali ya uchumi alisema "kwa jumla hali ya uchumi wa nchi yetu kwa mwaka 2008 ilikuwa ya kiwango cha kuridhisha. [21]
halisi
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Haruna Lipumba anasema, ripoti hiyo si sahihi kulingana na hali halisi ya maisha ya Watanzania na kwamba imelenga zaidi katika kupotosha. [22]
hao
Alisema wakiwa katika harakati za kusafirisha mali hizo, walizingirwa na wananchi wenye hasira kali na wenzao wawili kupigwa vibaya hadi kufa na baadaye kuchomwa moto, wakati washitakiwa hao wawili waliokolewa na polisi na kufikishwa mahakamani kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha. [23]
hapo
Kwa hiyo, ofisi inaandaa utaratibu ili wale waheshimiwa wabunge ambao hawajazipata fomu hizo, sasa wazichukue kutoka Ofisi ya Spika mara moja na kuzirejesha hapo haraka inavyowezekana," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo ya Ofisi ya Bunge. [24]
hasa
Naomba Watanzania wenzangu wote na hasa wanasiasa wenzangu tuyatambue hayo na tujiepushe nayo. [25]
hata
Vitendo hivyo havitavumiliwa hata kidogo. [26]
hicho
Mgombea wa Chadema, Sambwee Shitambala ameenguliwa kwenye kinyang'anyiro hicho cha kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mbunge wa CCM, Richard Nyaulawa, aliyefariki kwa ugonjwa, lakini amekata rufaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambayo inatarajiwa kutangaza uamuzi kesho. [27]
hii
Leo hii tukisema wangapi wanamuunga mkono Mkapa tutawapata wengi kuliko wachache wanavyofikiri. [28]
hofu
Kitendo cha wamiliki wa vituo vya mafuta kinapaswa kukemewa kwani wanawasababishia wananchi hofu ya maisha. [29]
huduma
Rais pia alisema serikali imekusudia kulifanyia marekebisho shirika hilo katika mwaka 2009, ili liweze kutoa huduma ipasavyo. [30]
huo
Naomba makundi ya kijamii yatambue ukweli huo na waache kuwaendekeza wanasiasa hasidi. [31]
huu
Ni ukweli ulio wazi kuwa katika mwaka huu tunaoumaliza sasa baadhi yetu tumekuwa tunafanya vitendo au kutoa kauli ambazo zilikuwa zinalielekeza taifa kubaya," alisema Kikwete. [32]
ikiwa
Tunaumaliza mwaka nchi ikiwa tulivu. [33]
juu
Sakata hilo la Richmond liliamsha ari na mwamko wa hali ya juu wa kisiasa kwa Watanzania na la kushangaza zaidi ni pale wabunge hata wale wa kutoka chama tawala waliposimama kidete kutetea maslahi ya taifa kinyume na walivyokuwa wakifanya huko nyuma. [34]
juzi
Hakimu magori alitoa hukumu hiyo juzi baada ya kuridhika na ushahidi uliowasilishwa mahakamani na upande wa mashitaka. [35]
kashfa
Lowassa hakujiuzulu peke yake, bali aliambatana na mawaziri Nazir Karamagi aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini na Dk Ibrahim Msabaha aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki kufuatia kuhusishwa kwao katika kashfa ya Richmond. [36]
kazi
Akizungumzia mauaji ya albino Rais Kikwete alisema serikali inaendelea na mapambano kuhakikisha inatokomeza mauaji hayo na kwamba imeunda kikosi kazi kuendesha mapambano hayo. [37]
kiasi
KOCHA wa Taifa Stars, Marcio Maximo amesema kuwa majina ya nchi na historia zao za nyuma hazimpi taAbu kiasi cha kumfanya ashindwe kufanya vizuri wakati wa michuano ya Afrika ya wachezaji wa ligi za ndani(CHAN) iliyopangwa kufanyika Februari mwakani nchini Ivory Coast. [38]
kila
Tutafanya kila tuwezavyo kurekebisha mambo ili huduma hizo ziboreshwe na kuwafanya watumiaji kufurahi. [39]
kina
Hivi sasa wanaendelea na uchunguzi wa kina nchi nzima kuwatambua wahalifu na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria. [40]
kinga
Wakati shinikizao la kutaka Mkapa aondolewe kinga na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za makosa anayodaiwa kufanya akiwa Ikulu, wabunge na wananchi wa mkoani Mtwara na wananchi kuibuka na kumtetea. [41]
kisiwa
Katibu wa Ujumbe wa watu walikwenda kuwasilisha barua ya madai hayo kwenye Ofisi za Mwakilishi Mkazai Umoja wa Mataifa, Hamad Ali Mussa alisema wanataka kisiwa hicho kiwe na mamlaka yake kama vilivyo visiwa vinavyounda utawala wa Comoro. [42]
kiti
Alisema kuwa katika kikao hicho cha halmashauri kilichofanyika jana, wamejipanga kuhakikisha kila mbunge anapangiwa majukumu yake katika kuhakikisha CCM inatetea vizuri kiti hicho kilichoachwa wazi na mbunge wake, Richard Nyaulawa. [43]
kocha
Baada ya mchezo huo, kocha mkuu wa Zambia, Herne Renald alilalamika uwanja wa Bugembe kuwa ni mbovu na mkavu akiulinganisha na ule wa Chuo Kikuu cha Zambia. [44]
kucheza
Alisema kuwa kutokana na wachezaji wengi wa Simba na Yanga kuwa katika timu ya Kilimanjaro Stars ambayo inashiriki michuano ya Chalenji inayoendelea Uganda na kuisha Januari 13,mechi za klabu hizo, zilizotakiwa kucheza Januari 10, sasa zitachezwa Januari 21 kwa Simba kucheza na Villa Squad na Yanga itacheza na Prisons mjini Mbeya. [45]
kufikishwa
Tayari watu 91 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani. [46]
kujiuzulu
Tukio kubwa kabisa mwaka huu ni lile la kujiuzulu Waziri Mkuu Edward Lowassa. [47]
kuna
Mulla alisema kuwa, endapo kuna vyama vya upinzani vitatimiza lengo lao la kumkashifu kiongozi huyo, CCM haitakubali kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai na hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa. [48]
kuomba
Kabla ya kuomba hela ya soda, Rama aliulalamikia upande wa mashitaka kwa kuchelewa kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo. [49]
kuwa
Hii inathibitisha kuwa nchi inaweza kuwa tulivu isipokuwa pale ambapo baadhi yetu tutakapokuwa tumeamua kuwa isiwe hivyo. [50]
kwao
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kila timu ikitaka ama kuongeza bao au kusawazisha, lakini milango ilikuwa ni migumu na mabekiwa timu zote walikuwa makini kuondoa hatari zilizoekekezwa kwao. [51]
la
Katika mwaka 2008 uliomalizika jana taifa lilishuhudia matukio mbalimbali- maandamano na migomo ya wafanyakazi, wanafunzi wa vyuo vikuu, wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, mapigano ya kikabilila mkoani na fujo katika kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Tarime mkoani Mara. [52]
licha
Sisi hatuwezi kuchukua polisi na kwenda kuwakamata licha ya ukweli kuwa ongezeko hilo linawaumiza wananchi. [53]
ligi
Alisema ratiba ya raundi ya pili imezingatia mashindano mbalimbali kama klabu bingwa Afrika na shirikisho, michuanio ya fainali ya wachezaji wanaocheza ligi ya ndani ( CHAN). [54]
madai
Askari hao walijitambulisha kwa mama huyo na kumtaka awaruhusu kufanya upekuzi ndani ya nyumba kitendo ambacho mama huyo alikipinga vikali kwa madai kuwa mumewe hayupo, lakini Polisi walimuhakikishia usalama wa mali zake hata hivyo mke huyo aligoma kabisa kuwaruhusu kuingia ndani kwa upekuzi. [55]
maendeleo
Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alisema jana kuwa katika kikao hicho walijadili mambo muhimu ya maendeleo ya soka la Afrika Mashariki na Kati. [56]
mafanikio
Matumani hayo kwa kiasi kikubwa yalichochewa na mafanikio ya kuwa na nguvu ya pamoja iliyochangia kukiondoa madarakani chama cha KANU nchini Kenya na kukiingiza chama kilichokuwa na muunganiko wa vyama mbalimbali vya upinzani nchini humo cha NARC Kenya. [57]
makubwa
Hata hivyo, kocha huyo alisema pamoja na matumaini makubwa aliyonayo kwa kikosi chake, bado Watanzania watatakiwa kuiunga mkono hata pale michuano hiyo itakapoanza akiwataka wale wenye uwezo wa kusafiri kufanya hivyo ili kwenda kuishangilia timu hiyo. [58]
mama
Ramadhan na mama yake Hadija Ally wanadaiwa kuwa Aprili 24 mwaka huu walimuua mtoto Salome Yohana (3) ambapo Rama alikamatwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwa na kichwa cha mtoto huyo. [59]
mambo
Ni matumaini yangu kuwa tutajiepusha na mambo hayo katika mwaka 2009. Nawasihi viongozi wenzangu wa kisiasa na wa kijamii tubadilike, tuweke mbele maslahi ya taifa ili tuiepushe nchi yetu na mabalaa ambayo baadhi ya wenzetu yaliwakuta. [60]
maoni
Mbunge wa jimbo la Mtwara, Mohamed Sinani alizungumzia suala hilo kidiplomasia zaidi, lakini akashindwa kuficha msimamo wake kwa Rais Mkapa, ambaye aliteuliwa na CCM kuwania urais baada ya kumshinda Rais Jakaya Kikwete katika marudio ya kura za maoni. [61]
mara
Alisema kuwa, mara nyingi kumekuwepo kambi za vijana wa CCM kwa ajili ya kujifunza itikadi za chama hicho na kwamba kambi hiyo ni kwa ajili ya shughuli za vijana. [62]
masikini
Lipumba anafafanua kuwa, ripoti hiyo inatofautiana na ripoti ya serikali ya Novemba/Desemba mwaka huu, ambayo yenyewe inaonyesha kuwa watu masikini wameongezeka kutoka 11.7 milioni 2005 hadi 12.7 milioni 2007, na kuongeza kuwa kuna ongezeko la watu milioni moja ambao ni masikini. [63]
matatizo
Yapo matatizo ya uendeshaji ambayo yamesababisha huduma zitolewazo ATCL kuwa za kiwango kisichoridhisha,” alisema Rais Kikwete. [64]
mauzo
Baadhi ya viashiria vilivyoainishwa katika ripoti hiyo kuwa vimefanikiwa sana ni pamoja pato la taifa, pato la serikali, mauzo ya nje, pato la mtu mmoja mmoja na miradi mipya iliyofunguliwa na kusajiliwa. [65]
meli
WAAGIZAJI wakubwa wa mafuta nchini wamewakana na wamiliki wa vituo vya kuuza nishati hiyo na kushangazwa na kitendo cha kupandisha bei kiholela wakati wa sikukuu ya Krismas kwa kisingizio cha uadimu wa mafuta baada ya meli kuzuiwa na maharamia wa Kisomali. [66]
mfumuko
Profesa Lipumba anasema kwamba hali ya mfumuko wa bei inayotangazwa katika ripoti mbalimbali za serikali ni mara mbili zaidi ya hali halisi ya mfumuko wa bei za bidhaa muhimu nchini. [67]
mgomo
Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, latangaza kuwasimamisha masomo kwa muda usiojulikana, wanafunzi wa shahada ya kwanza kufuatia mgomo waliouitisha kuishinikiza serikali iwaongezee fedha za mikopo. [68]
mke
POLISI wilayani hapa wanamshikilia mkazi wa kitongoji cha Kobhetimo kijiji cha Nyansurumuti kata ya Kisaka tarafa ya Ngoreme maarufu kwa majina ya Mrema Mantago Nkoba (28) kwa tuhuma za kumchoma kisu na kusababisha kifo cha mdogo wake baada ya kumtuhumu kuwa na uhusiano wa mapenzi na mke wake. [69]
mpya
Kuhusu utekelezaji wa kazi za Bunge kwa mwaka huu mpya wa 2009, Spika Sitta alisema atahakikisha unafuata katiba na sheria. [70]
mtu
Katika tukio jingine, jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa tukio moja la kuuawa mtu mmoja kwa tuhuma za kuiba gunia mbili za mpunga, katika kijiji cha Ihalo kata ya Kwesela wilaya ya Shinyanga. [71]
mwa
Miongoni mwa tuhuma za Mkapa, ambaye anasifika kwa kuinua uchumi baada ya kuukuta kwenye hali mbaya, ni kujiuzia mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mkoani Mbeya kwa bei nafuu akitumia kampuni ya Tan Power Resources anayoimulika pamoja na waziri wa zamani wa nishati na madini, Daniel Yona wakati akiwa rais. [72]
mwisho
Spika Sitta alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na gazeti hili kuhusu urejeshwaji wa fomu hizo ambao tarehe yake ya mwisho ilikuwa jana. [73]
nane
WAKATI Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) likikamilisha mpango maalum wa kuinua kiwango cha mchezo huo, utekelezaji wake unatarajia kukamilika baada ya miaka nane, imeelezwa. [74]
nao
Kamanda huyo alisema baada ya mzozo wa muda mrefu kama wa dakika 10 hivi mama huyo aliamua kuwaruhusu kufanya upekuzi huku akishirikiana nao kwa kuwafungulia chumba kimoja baada ya kingine na ndipo walipokuta fuvu hilo likiwa limehifadhiwa kwenye ndoo kidogo ikiwa imefunikwa na mafuta mengi ya samli ili isionekana kama kuna kitu kingine zaidi ya samli hiyo. [75]
naye
Morumbe Mantago(22) ambaye ni mdogo wake naye mkazi wa kijijini hapo. [76]
ndio
Tunaangalia jinsi ya kuiandaa Taifa Stars kwa vile ndio inawakilisha ukanda wetu na kikao kimeshauri kwamba timu hiyo ipatiwe maandalizi ya kutosha ili ituwakilishe sawasawa,îalisema Musonye. [77]
ndiyo
Sitta aliongeza kuwa, wamewasiliana na Ofisi ya Kamishna wa Maadili na kueleza hali hiyo na ndiyo sababu ofisi yake imetoa tamko kuwataka wabunge wasiopata fomu hizo kuzifuata ofisini kwake. [78]
nje
Alisema baada ya kukuta fuvu hilo polisi walikitoa kindoo hicho nje ambako muda huo tayari majirani na watu wengine waliosikia uwepo wa tukio hilo waliwa wameshafika kushuhudia upekuzi huo na askari waliwaruhusu kuangalia ndani ya sadolini hiyo ili waweze kuona kilichokuwa kikifanyika ndani ya nyumba hiyo. [79]
nne
Hatari yake ni kwamba wanafunzi watakaopitia mazingira hayo watamaliza kidato cha nne bila ya kuwa na elimu inayolingana na kiwango hicho. [80]
rais
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Mbeya,kimevionya vyama vya upinzani vyenye lengo la kumchafua rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Mbeya Vijijini. [81]
rasmi
Mgeni rasmi katika mchezo wa Uganda na Zanzibar atakuwa Janet Museveni, mbunge na mke wa Rais Yoweri Museveni. [82]
ripoti
Kwa mujibu wa ripoti hiyo serikali inajigamba na kujinasibu kuwa uchumi wa Tanzania unapeta ndani ya kipindi hicho cha miaka mitatu. [83]
saa
Aidha habari ambazo gazeti hili imezipata kutoka ndani ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinasema rufaa ya Shitambala itatolewa leo saa 4:00 asubuhi. [84]
sisi
Siku chache kabla ya sikukuu ya Krismasi baadhi ya wafanyabiashara walihofia kutokea kwa uhaba wa mafuta baada ya kuwepo taarifa kwamba nchi jirani hazina mafuta, hivyo wakalazimika kupandisha bei ya bidhaa hiyo kiholela ingawa sisi kwa ujumla wetu kila mmoja ana akiba itakayoweza kutumika kwa siku 25 na kabla hayajamalizika meli za mafuta zitakuwa zimeshawasili nchini," alisema Hirani. [85]
soko
Alisema serikali itatumia nguvu nyingi katika kuhami na kukuza uchumi na kwamba,serikali itaendelea kushirikiana na Benki Kuu kuzuia athari za soko la fedha duniani zisilifikie taifa na iwapo zitalifikia, makali yake yawe nafuu. [86]
tamaa
Msemo huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuinua maendeleo ya watu mbalimbali hasa pale kunapoonekana kuna vikwazo ambavyo vinakatisha tamaa, na hivyo kufanya baadhi ya watu au kikundi cha watu kuanza kujitenga kwa ama kukatishwa tamaa, ama kuona mambo hayatakuwa kama wanavyofikiria. [87]
tangu
Hapa nchini tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, kumekuwa na ushindani dhaifu dhidi ya chama tawala CCM katika chaguzi zote zilizofanyika tangu mwaka 1995 ulipofanyika uchaguzi mkuu chini ya mfumo wa vyama vingi. [88]
tena
Hakimu huyo aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 14 mwakani itakapotajwa tena. [89]
timu
Mwakyoma alisema taarifa hizo timu ya askari ilitembelea eneo la nyumba hiyo ambapo hata hivyo hawakufanikiwa kumkuta mfanyabiashara huyo na badala yake walimkuta mke wake aitwaye Mwanaidi Ramadhani (25). [90]
tuna
Hakuna mgawanyiko ndani ya chama chetu cha CCM na hakuna wabunge waliogawanyika wote ni kitu kimoja na tumejipanga vizuri na tunamwomba Mwenyezi Mungu atusaidie ili tuweze kupata ushindi kwa asilimia kubwa na tuna imani kuwa tutashinda," alisema. [91]
ufisadi
Meghji na Mramba, wamepoteza nyadhifa zao wiki chache baada ya kuibuka kashfa ya ufisadi wa mabilioni ya shilingi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo ni taasisi ya umma iliyo chini ya wizara waliyokuwa wakiiongoza kwa nyakati tofauti. [92]
ule
Katika maelezo yake, Spika Sitta alisema kuwa mfumo uliotumika mwaka jana kuwafikishia wabunge fomu hizo kwa kuzituma majimboni mwao umesababisha usumbufu, tofauti na ule wa miaka iliyopita wakati wabunge walipokuwa wakigawiwa fomu hizo kwenye kikao chao cha mwezi Novemba. [93]
umma
Rais alitaja taasisi nyingine za umma ambazo utendaji wake ulikuwa mbaya ni Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA). [94]
wa
Rais alitoa onyo hilo katika hotuba yake ya salaam za Mwaka Mpya wa 2009 kwa wananchi, aliyoitoa jana kupitia vyombo vya habari, akizungumzia changamoto kadhaa za mwaka 2009 na mikakati ya serikali yake kukabiliana nazo baada ya mikakati ya mwaka 2008 kuathiriwa na kuporomoka kwa uchumi wa nchi tajiri kutokana na kuyumba kwa taasisi za kifedha. [95]
wala
Suala la mafuta kupanda ni suala la wamiliki wa vituo vya mafuta wala halihusiani na sikukuu za Krismas ama sisi kufunga ofisi wakati wa sikukuu na wala lisihusishwe na suala la maharamia wa Kisomali, bali ni maamuzi ya wamiliki wa vituo vya mafuta ya kupandisha bei kwa sababu wanazozifahamu. [96]
wao
Alizungumza masuala mengi yakiwemo ya sheria zilizotumika kumuondoa na akazikosoa na hatimaye aliwataka wananchi wawe wavumilivu, hata kama rufaa yao haitakubaliwa kwa kuwa atawaachia wananchi wenyewe waamue hatima ya mustakabali wao ingawa pia aliwahakikishia kuwa haki yao lazima wataipata. [97]
wengi
PAMOJA na kuwekewa pingamizi na hatimaye kuenguliwa kwa mgombea wake wa ubunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kiliendelea kupiga kampeni katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na watu wengi. [98]
wetu
Navionya vyama vya upinzani vinavyosema kuwa vitamkashifu rais wetu mstaafu wa awamu ya pili wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi katika jimbo la Mbeya Vijijini, kuwa hatutakubaliana na vitendo hivyo. [99]
zao
WABUNGE wametakiwa kurejesha fomu za tamko la mali zao walizopatiwa na Ofisi ya Kamishna wa Maadili ndani ya siku 14 kuanzia leo, Spika wa Bunge Samuel Sitta amesema. [100]
  NODES
Note 1