Machi

mwezi wa tatu katika mwaka
Feb - Machi - Apr
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30 31
Kalenda ya Gregori

Mwezi wa Machi ni mwezi wa tatu katika Kalenda ya Gregori. Jina lake limetokana na jina la mungu wa vita wa Warumi Mars.

Tarehe 20, mwezi huo wa Machi, ni siku mlingano (au ikwinoksi kutoka Kiingereza equinox) ambapo jua huvuka mstari wa ikweta, na usiku na mchana ziko sawasawa kimuda duniani popote (ila maeneo ya ncha ambapo nusu ya jua hubaki chini ya upeo wa macho na nusu nyingine juu kwa siku nzima).

Machi ina siku 31, na inaanza na siku ya juma sawa na mwezi wa Novemba, na pia katika miaka ya kawaida isiyo mirefu, siku yake ya kwanza ni sawa na mwezi wa Februari.

Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
  NODES