Ujuzi maana yake ni kufahamu, kujua na kuelewa hali, habari na maelezo yanayohusu mazingira tunapoishi. Tunapata ujuzi kwa maarifa yetu au kwa njia ya kufundishwa tukitazama, kutambua, kulinganisha na kutafakari yale tuliyoona na kujifunza.

Mwanafalsafa Francis Bacon alisema "Ujuzi ni mamlaka" ("knowledge is power").

Kimsingi tunaona tofauti kati ya ujuzi na rai au hoja tupu. Rai na hoja zinakuja pamoja na hisia na maarifa ambayo mara nyingi haikutafakariwa kimakini. Kinyume chake ujuzi ni yale tunayoona kuwa yana kiwango kikubwa cha uhakika baada ya kujadiliwa na watu wengi katika mchakato unaoeleweka. Lakini kila ujuzi una kiwango cha kukosa uhakika kwa sababu uwezekano wa makosa katika kuelewa uhalisia unabaki kila wakati.

Katika falsafa, elimu ya jinsi ya kupata ujuzi huitwa epistomolojia. Mwanafalsafa Plato alieleza ujuzi kuwa "rai ya kweli yenye msingi mzuri" (kwa Kiingereza "justified true belief").

  NODES