Akropoli
Akropoli ilikuwa makazi ya sehemu ya juu ya mji wa kale wa Kigiriki, hasa ngome, na mara nyingi kilikuwa kilima chenye pande wima, kilichochaguliwa hasa kwa ajili ya ulinzi. Neno hili hutumika mara nyingi kumaanisha Akropoli ya Athene, ingawa kila mji wa Kigiriki ulikuwa na akropoli yake.
Akropoli zilitumika kama vituo vya kidini na sehemu za kuabudu, ngome, na makazi ya kifalme na wenye hadhi ya juu. Akropoli zilikuja kuwa kitovu cha miji mikubwa ya nyakati za kale za Kigiriki, na zilihudumu kama vituo muhimu vya jamii.
Baadhi ya Akropoli maarufu zimekuwa vituo vya utalii leo, na hasa Akropoli ya Athene imekuwa kitovu cha mapinduzi ya masomo ya Ugiriki ya kale tangu kipindi cha Mycenaean. Nyingi ya akropoli hizi zimekuwa chanzo cha mapato kwa Ugiriki, na zinawakilisha baadhi ya teknolojia kuu za kipindi hicho.[1]
Marejeo
hariri- ↑ Eyewitness: Ancient Greece. Eyewitness. ku. 30–40.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Akropoli kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |