Amosi
Amosi (kwa Kiebrania עָמוֹס, Amos) ni mmojawapo kati ya manabii wa Israeli. Kitabu chake, kutokana na ufupi wake, ni kati ya vile 12 vya Manabii Wadogo.
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Maisha na kazi
haririBaada ya unabii wa Eliya na Elisha, Mungu aliendelea kukazania ufalme wa kaskazini kabla haujaangamizwa kabisa: tahadhari kabla ya hatari.
Ndiyo sababu, ili kuthibitisha haki yake na utakatifu wake dhidi ya maovu ya Waisraeli, alimtuma huko Amosi kutoka Tekoa (ufalme wa kusini), alipokuwa mfugaji na mtunzaji wa mibuyu karibu na jangwa[2].
Amosi aliona maendeleo makubwa ya kaskazini chini ya mfalme Yeroboamu II, lakini hakudanganywa nayo, bali alitabiri yatakoma mapema.
Aliona Waisraeli wanaoshika sabato na sikukuu, pamoja na ibada na sadaka mbalimbali, lakini wananyanyasa wenzao maskini: hapo akapiga kelele kudai kwanza haki itiririke kama maji ya mto ili ibada ziwe na maana.
Hatimaye alikatazwa asiendelee kuhubiri, pia kwa sababu alikuwa mtu wa kusini, hivyo walifikiri anasema kwa kijicho tu.
Habari zake zinapatikana katika Kitabu cha Amosi ndani ya Tanakh (Biblia ya Kiebrania), kwa hiyo pia katika Agano la Kale la Biblia ya Kikristo.
Ni kwamba, tofauti na manabii Eliya na Elisha waliomtangulia wasiache maandishi, nabii Amos (786 - 746 hivi K.K.) ana kitabu chenye mafundisho yake aliyoyatoa katika ufalme wa Israeli (Kaskazini) ingawa alikuwa mtu wa ufalme wa Yuda (Kusini).
Hakutarajia kutumwa na Mungu, ila ilimbidi akubali kutabiri kwa niaba yake (7:10-17), hasa kuwa Israeli itaangamizwa na kutekwa na Waashuru utumwani kwa makosa dhidi ya imani na ya haki pamoja na anasa (5-6).
Waisraeli wakakataa maneno yake hata wakatendwa alivyowatabiria kwa ukali wote (2Fal 17:5-23).
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- Anderson, Bernhard W. & Foster R. McCurley The Eighth Century Prophets: Amos, Hosea, Isaiah, Micah Wipf and Stock: 2003. ISBN 1592443540
- Rosenbaum, Stanley Ned Amos of Israel: A New Interpretation Georgia: Mercer University Press: 1990. ISBN 0865543550
Viungo vya nje
hariri- The Holy Prophet Amos Orthodox icon and synaxarion
- Hypertext bible commentary: Amos Ilihifadhiwa 21 Novemba 2008 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Amosi kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |