Bata

(Elekezwa kutoka Anatidae)
Bata
Bata domo-njano
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Anseriformes (Ndege kama bata)
Familia: Anatidae (Ndege walio na mnasaba na bata)
Ngazi za chini

Nusufamilia 9:

Mabata ni ndege wa maji wa familia ya Anatidae wenye madomo mafupi na mapana na miguu yenye ngozi kati ya vidole. Manyoya yao huwa na uwezo bora wa kufukuza maji kwa msaada wa mafuta maalumu. Mabata ndiyo moja ya familia za ndege ambazo spishi zao zina uume, kwa sababu mabata wanapandana majini tu.

Mabata huchanganywa pengine na aina kadhaa za ndege wa maji wasiohusiana wenye maumbo yanayofanana, kama wazamaji, vibisi, kukuziwa na shaunge.

Mofolojia

hariri

Mwili wote wa mabata kwa ujumla ni mrefu na mpana, na mabata wengi kwa wastani wana shingo fupi lakini shingo la mabata bukini na mabata-maji ni ndefu. Umbo la mwili la mabata kwa kiasi fulani hutofautiana na hawa kwa kuwa kidogo wa duara kidogo. Miguu yenye magamba ni yenye nguvu na iliyokuwa vizuri, na kwa kawaida, na hurushwa nyuma kabisa ya mwili, hivyo zaidi hasa kwenye spishi za majini. Mbawa zake ni zenye nguvu na kwa ujumla ni ndogo na zilizochongoka, na kupaa kwa bata kunahitaji mapigo ya haraka bila ya kupumzika, hivyo kuhitaji misuli yenye nguvu sana. Hata hivyo spishi tatu za bata aina ya steamer hawawezi kuruka kabisa. Spishi nyingi za bata hushindwa kuruka vizuri kipindi cha kupukutisha manyoya ya zamani na kuotesha mapya; hutafuta mazingira salama yenye chakula kingi wakati huo. Hivyo basi kipindi hiki hufuata baada ya kipindi cha kuhama.

Ndege hawa wana rangi mbalimbali. Spishi kubwa hutafuta chakula aghalabu ardhini au kwa maji machache. Spishi ndogo nyingine hula mimea ya maji na huzamia kichwa chao tu, nyingine huzamia kabisa ili kukamata samaki, wanyamakombe au mimea ya maji, lakini spishi kadhaa hutafuta chakula ardhini. Hujenga matago yao ardhini, juu ya mwamba, ndani ya shimo la miti au ndani ya pango la sungura, mhanga, k.y.k.

Manyoya ya spishi kadhaa hupendwa sana kama kijazo cha mito, mifarishi, mafuko ya kulalia na makoti. Spishi nyingi za mabata hutumika kama chakula.

Wataalamu hawakubaliana kuhusu uainisho wa mabata ndani ya familia yao. Kuna ainisho mbalimbali na mmoja tu unaonyeshwa hapa:

Dendrocygninae: Mabata-miti

hariri
 
Bata-miti uso-mweupe

Mabata wenye miguu mirefu ambao wanafanana na mabata bukini. Jenasi moja itokeayo kila mahali pa kufaa nchini kwa tropiki:

Thalassorninae: Kotwe

hariri

Wana mnasaba na Dendrocygninae, lakini wanafanana na familia ndogo Oxyurinae. Jenasi moja kwa Afrika:

 
Bata-maji domo-fundo

Spishi 27 za mabata wakubwa ndani ya jenasi 7 ambazo zinatokea kanda za halijoto wastani hasa kaskazini mwa ikweta lakini spishi chache kusini mwa ikweta (spishi kadhaa, kama bata-maji domo-fundo, zimewasilishwa kwa Afrika):

Stictonettinae: Bata madoadoa

hariri
 
Bata madoadoa

Jenasi moja kwa Australia ambayo ilikuwa imeainishwa zamani ndani ya Oxyurinae, lakini anatomia yake ionyesha mnasaba na Anserinae:

Jenasi moja kwa Afrika ambayo ilikuwa imeainishwa zamani kama 'bata anayetua', lakini iko karibu zaidi na Tadorninae:

 
Bata bukini wa Misri

Jamii hii ya mabata makubwa wanaotokea mara nyingi nchini kavu ni kati ya Anserinae na Anatinae. Juzijuzi wataalamu wameainisha jenasi 10 na spishi 23 (moja imekwisha labda) ndani ya familia ndogo hii, nyingi zaidi kutoka kusini mwa ikweta:

Anatinae: Mabata wachovya na wazamaji na moa-nalo

hariri
 
Bata bawa-kijani

Jamii ya mabata wachovya ambao wanatokea sehemu zote duniani ilikuwa imeainishwa kwa jenasi mbili tu, lakini ina jenasi 8 sasa na spishi 55:

 
Bata domo-jembamba

Jamii ya mabata wazamaji ambao wantokea sehemu zote duniani ina spishi 16 ndani ya jenasi 3. Marmaronetta ilikuwa imeainishwa zamani miongoni mwa mabata wachovya lakini inaainishwa hapa sasa.

Jamii ya moa-nalo (jina kwa Kihawaii) ni ya pekee. Mabata hawa walitokea Hawaii lakini wamekwisha sasa. Walikuwa wakubwa sana na domo nene sana na walifanana na mabata bukini ambao hawakuweza kuruka angani. Walikuwa na mnasaba na jenasi Anas.

 
Bata-domomeno kidari-chekundu

Familia ndogo hii ina spishi 20 (moja au mbili zimekwisha). Spishi nyingi zaidi zinatokea kaskazini mwa ikweta, lakini kuna spishi mbili za Mergus kusini mwa ikweta.

 
Bata kichwa-cheupe

Jamii ndogo ya mabata iliyo na spishi 8 ndani ya jenasi 4:

Spishi za Afrika

hariri

w:en:File:Duck 1 filter teeth edit.jpg Utando wa Pecten mdomoni

Bata hula aina mbalimbali ya chakula kama vile kama vile nyasi, mimea ya majini, samaki, wadudu, amfibia wadogo, minyoo na moluski. Bata wanaoogelea na bata wa baharini wanakula wanyama chini kabisa ya kina cha maji. Ili kuweza kuzama kwa urahisi, bata wanaoogelea ni wazito kuliko bata aina ya dabbling, hivyo inakuwa vigumu kwa wao kuruka. Bata hawa wa dabbling hula kwenye uso wa maji au ardhini, au chini ya ardhi kwa kadiri ya uwezo atakaoweza kufikia bila ya kuzama kabisa.[4] Kuzunguka mdomo wa bata kuna umbo mithili ya kitana, iitwayo pecten. Hii huchuja majimaji kwa kuyapitisha kwenye pande za mdomo na kubakiza chakula chochote ndani. Pecten pia hutumika kupuna manyoya. Baadhi ya spishi kama vile smew, goosander na mergansers wanauwezo wa kumeza samaki wakubwa. Bata wengine wana midomo bapa mahsusi kwa kazi za kuzoa na kuvuta kama vile kuvuta magugumaji, kuvuta minyoo na moluski nje ya matope, kutafuta lava wa wadudu, na kazi kubwa.

Marejeo

hariri
  1. ^ "Duckling". The American Heritage Dictionary of the English Language, Fourth Edition Copyright 2006 by Houghton Mifflin Company. Republished by dictionary.com, http://dictionary.reference.com/browse/duckling, Accessed 05-01-2008.
  2. ^ "Duckling". Kernerman English Multilingual Dictionary (Beta Version), 2000-2006 K Dictionaries Ltd., Republished by dictionary.com, http://dictionary.reference.com/browse/duckling, Accessed 05-01-2008.
  3. ^ Photo of a duck eating a frog
  4. ^ Ogden, Evans. "Dabbling Ducks". CWE. http://www.sfu.ca/biology/wildberg/species/dabbducks.html. Retrieved 2006-11-02.
  5. ^ Amos, Jonathan. "Sound science is quackers". BBC News. http://news.bbc.co.uk/2/hi/science/nature/3086890.stm. Retrieved 2006-11-02.
  6. ^ "Mythbusters Episode 8". 12 Desemba 2003. http://mythbustersresults.com/episode8.
  7. ^ "Mallard - Nature Notes". Ducks Unlimited Canada. http://www.ducks.ca/resource/general/naturenotes/mallard.html Ilihifadhiwa 25 Machi 2011 kwenye Wayback Machine.. Retrieved 2006-11-02.

Viungo vya Nje

hariri
  • Wild Ducks Info – Maelezo ya kina kuhusu bata wa mwituni.
  • Duck videos kwenye Mkusanyiko wa Ndege kwenye Wavuti.
  • list of books (sehemu bora ya kutazama)
  • Ducks at a Distance, by Rob Hines at Project Gutenberg - Mwongozo wa kisasa wa kuwatambua bata maji wa Marekani.

Imerekebishwa kutoka w:en:Duck

  NODES
chat 1
Note 2
Project 1