Anemia
Anemia (kutoka Kiingereza; katika lugha hiyo inaandikwa pia anaemia) ni ugonjwa wa kukosa idadi ya kutosha ya seli nyekundu za damu (upungufu wa hemoglobini katika damu).[1][2]
Anemia | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Matamshi | |
Kundi Maalumu | Hematology |
ICD-10 | D50.-D64. |
ICD-9 | 280-285 |
DiseasesDB | 663 |
MedlinePlus | 000560 |
eMedicine | med/132 emerg/808 emerg/734 |
MeSH | D000740 |
Kwa lugha nyingine, anemia ni uwezo mdogo wa damu kusafirisha oksijeni mwilini.[3]
Kama anemia inaanza polepole dalili zake mara nyingi ni dhaifu, zikiwa pamoja na uchovu, udhaifu na ugumu wa kupumua.
Anemia inayoanza ghafla ina dalili kali zaidi, zikiwa pamoja na kuchanganyikiwa akilini, kujisikia kama karibu na kupotea, ufahamu au kupotea ufahamu kweli, au kiuu kikali. Kama anemia imeendelea watu weupeweupe wanaweza kuonekana weupe zaidi kuliko kawaida; Waafrika mara nyingi huonyesha rangi ya njano chini ya kucha. Additional symptoms may occur depending on the underlying cause.[4]
Aina za anemia
haririKuna hasa aina 3 za anemia
- Kutokana na upotevu wa damu
- kutokana na upungufu wa uzalishaji wa seli nyekundu za damu mwilini
- kutokana na uharibifu wa seli nyekundu katika damu.
Sababu za upotevu wa damu ni pamoja na jeraha, hasa jeraha ndani ya utumbo.
Sababu za upungufu wa uzalishaji wa seli nyekundu ni uhaba wa chuma, uhaba wa vitamini B12 na matatizo ndani ya uboho wa mifupa unaozalisha seli hizi.
Uharibifu wa seli nyekundu za damu husababishwa na anemia selimundu, magonjwa kama malaria na mengine
Marejeo
hariri- ↑ "What Is Anemia? - NHLBI, NIH". www.nhlbi.nih.gov. Iliwekwa mnamo 2016-01-31.
- ↑ Stedman's medical dictionary (tol. la 28th). Philadelphia: Lippincott Williams & Wilkins. 2006. uk. Anemia. ISBN 9780781733908.
- ↑ Rodak, Bernadette F. (2007). Hematology : clinical principles and applications (tol. la 3rd). Philadelphia: Saunders. uk. 220. ISBN 9781416030065.
- ↑ Janz, TG; Johnson, RL; Rubenstein, SD (Nov 2013). "Anemia in the emergency department: evaluation and treatment". Emergency medicine practice. 15 (11): 1–15, quiz 15-6. PMID 24716235.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Anemia kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |