Askofu mkuu

(Elekezwa kutoka Askofu Mkuu)

Askofu mkuu ni cheo cha askofu kiongozi anayesimamia maaskofu katika jimbo la kanisa lenye dayosisi mbalimbali.

Asili ya neno lenyewe ni Kigiriki αρχή arché (mwanzo, wa kwanza). Sehemu ya pili ni neno la Kigiriki επίσκοπος episkopos (mwangalizi) lililofikia Kiswahili kupitia umbo la Kiarabu uskuf.

Kanisa katoliki

hariri

Kama nchi ina wakatoliki wengi kuna majimbo mbalimbali na kila moja ina askofu mkuu wake. Kama idadi ya wakatoliki ni wastani huwa na jimbo moja na askofu mmoja tu mwenye cheo cha askofu mkuu.

Waanglikana na Walutheri

hariri

Katika makanisa mengine huwa askofu mkuu ni askofu kiongozi wa nchi fulani. Lakini cheo hiki hakitumiwi vile katika kila nchi na Walutheri ni hasa Walutheri wa Uswidi, Ufini, Urusi na Estonia walio na askofu mkuu.

  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Askofu mkuu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES