Bamba la Ulaya-Asia
Bamba la Ulaya-Asia ni bamba la gandunia kubwa katika ganda la dunia. Inabeba sehemu kubwa ya bara za Ulaya na Asia isipokuwa Bara Hindi na mashariki mwa Siberia si sehemu zake. Kwa lugha nyingine inawezekana kusema inabeba Eurasia.
Limepakana na bamba la Amerika Kaskazini, bamba la Australia, bamba la Uhindi, bamba la Uarabuni na bamba la Afrika.