Barafuto huitwa pia "mto wa barafu". Ni kanda kubwa la barafu iliyoanza kutambaa kutokana na uzito wake ikifuata graviti kwenye mtelemko. Kwa sababu hiyo barafuto zinapatikana hasa mlimani.

Barafuto

Asili ya barafu ya barafuto

hariri
 
Barafuto ndogo juu ya mlima Kilimajaro

Barafuto zimetokana na theluji inayokaa miaka mingi bila kuyeyuka katika mazingira baridi. Theluji mpya inakaa juu ya theluji ya miaka iliyotangulia. Uzito wa theluji ya baadaye inakandamiza ile ya chini. Kutokana na shindikizo hili theluji ya chini hubadilika kuwa barafu kabisa.

 
Bonde lenye umbo la "U" lilikatwa na barafuto huko Mt. Hood, Marekani

Barafuto ni kati ya nguvu kubwa za mmomonyoko duniani.

Afrika ina barafuto ndogo kadhaa juu ya mlima Kilimanjaro na mlima Kenya lakini zinaelekea kupotea kutokana na uhaba wa mvua itakayobadilika kuwa theluji mpya.

 
Barafuto ya Aletsch, Uswisi yenye umbo la mto wa barafu

Zamani za enzi ya barafu kiwango cha barafu kwenye ncha ya kaskazini kilikuwa kikubwa kiasi cha kusababisha barafuto kutokea zilizosukuma barafu hadi Ulaya ya Kati.

  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

  NODES