Basilika ni jina la heshima kwa ajili ya kanisa fulani katika Kanisa Katoliki.

Basilika la Salta.
Muundo wa basilika hili unaonyesha ukumbi mkuu katikati na kumbi za kando kati ya nguzo na ukuta wa pembeni.

Asili ya basilika

hariri

Kwa asili lilikuwa jengo rasmi lililotumika huko Roma ya Kale kama mahali pa mikutano ya hadhara na maamuzi ya kimahakama.

Jina ni la Kigiriki (aulè basilikè, yaani ukumbi wa kifalme), hivyo linaelekeza kuona asili ya majengo hayo upande wa mashariki wa Bahari ya Kati

Basilika kama jengo la kanisa

hariri

Kuanzia mwaka 313, Dola la Roma liliporuhusu raia kufuata Ukristo, mabasilika yaligeuzwa kuwa mahali pa ibada ya dini hiyo, kuanzia Kanisa kuu la Roma, maarufu kwa jina la Mt. Yohane huko Laterani.

Baadaye yakajengwa Basilika la Mt. Petro huko Vatikani, Basilika kuu la Bikira Maria na Basilika la Mt. Paulo nje ya kuta za jiji.

Baadaye tena, cheo cha Basilika kilitolewa kwa makanisa mengimengi kutokana na umuhimu wake upande wa historia, dini na sanaa.

Hata hivyo, kuna basilika kuu na basilika dogo.

 
Muundo wa basilika lenye kumbi 5

Basilika kama mtindo wa pekee wa ujenzi

hariri

Katika fani ya historia ya usanifu ni jina kwa ajili ya kanisa lililojengwa kwa kufuata mtindo wa pekee. Hapo kanisa huwa na ukumbi mkuu na kando yake sehemu iliyotengwa kwa nguzo. Mara nyingi muundo huo ulikuwa na kumbi mbili za kando lakini kuna pia basilika kubwa zenye kumbi 2 za kando kila upande kwa hiyo jumla 5.

  Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Basilika kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES