Chama cha Kikristo cha Kidemokrasia cha Ujerumani

(Elekezwa kutoka CDU)

Chama cha Kikristo cha Kidemokrasia cha Ujerumani (kwa Kijerumani: Christlich Demokratische Union Deutschlands; kifupisho: CDU) ni kimojawapo kati ya vyama viwili vikubwa vya kisiasa nchini Ujerumani. Kinajielezea chenyewe kuwa:

Christlich Demokratische Union Deutschlands
CDU logo
CDU logo
Kiongozi Armin Laschet
Kimeanzishwa 1870 (Kama Centre Party)
1945 (CDU)
Makao Makuu Klingelhöferstraße 8
10785 Berlin
Itakadi ya Chama Christian Democracy, Conservatism
Ushirikiano wa Kimataifa Christian Democrat International na International Democrat Union
Ushirikiano kwa Ulaya {{{Ulaya}}}
Kundi la Ubunge wa Ulaya {{{bunge la ulaya}}}
Rangi Black, Orange
Tovuti www.cdu.de
Tazama pia Siasa ya Ujerumani

Vyama vya Kisiasa
Uchaguzi


chama cha kisiasa kilicho cha Kikristo, cha kidemokrasia, cha uhuru na cha mapokeo, chenye msimamo wa kati ya eneo la kisiasa.

Mnamo mwezi Novemba katika mwaka wa 2005 Angela Merkel amepata kuwa Chansela wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kwa kupitia kiti cha chama cha CDU.

Chama na dini

hariri

Kihistoria CDU ilianzishwa kama maungano ya mikondo ya Kikatoliki na Kiprotestanti ya kisiasa ya Kijerumani baada ya vita kuu ya pili ya dunia.

Kabla ya utawala wa Adolf Hitler mikondo hii iliendelea kandokando hadi mwaka 1933; chama cha Zentrum kilikuwa chama cha Kikatoliki na vyama vya kiprotestanti vilijipasua hadi kupotea.

Baada ya vita ilikua nia ya wanasiasa Wakristo kuungana na kuwa na sauti moja, hivyo waliunda CDU. Kwa miaka mingi uwiano kati ya wanasiasa Wakatoliki na Waprotestanti ulikuwa jambo muhimu ndani ya chama.

Katika miaka ya nyuma CDU imejitahidi kukusanya pia Waislamu Wajerumani hasa kutoka wahamiaji Waturuki na watoto wao. CDU imekuwa chama cha kwanza katika Ujerumani kilichomteua waziri Mwislamu kwenye ngazi ya serikali ya jimbo la Saksonia ya chini mwaka 2010.

  NODES
INTERN 2