Chuo Kikuu cha Oxford

Chuo Kikuu cha Oxford (kwa kifupi Oxford) ni chuo kikuu cha utafiti nchini Ufalme wa Muungano, kilichoanzishwa mnamo mwaka 1096 huko Oxford, Uingereza. Hiki ni chuo kikuu cha kale kabisa katika ulimwengu unaotumia lugha ya Kiingereza na chuo kikuu cha pili duniani cha kale kinachoendelea kufanya kazi. Chuo hiki kilikuwa kwa kasi wakati Mfalme Henry wa Pili alipokataza wanafunzi wa Uingereza kuhudhuria Chuo Kikuu cha Paris. Baada ya mgogoro kati ya wanafunzi na wakazi wa mji wa Oxford mwaka 1209, baadhi ya wanataaluma walikimbilia Cambridge ambapo walianzisha Chuo Kikuu cha Cambridge. Vyuo hivi vikuu vya kale mara nyingi hujulikana kama "Oxdridge".

Radcliffe Camera.

Chuo kikuu hiki kinajumuisha taasisi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vyuo vikuu vishiriki 39 vyenye na idara mbalimbali za kitaaluma ambazo zimepangwa katika makundi manne. Vyuo vyote ni taasisi za kujitegemea ndani ya chuo kikuu, kila mmoja kikidhibiti uanachama wake na kwa muundo wake wa ndani na shughuli zake.

Viungo vya Nje

hariri
 
WikiMedia Commons
  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Oxford kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
Done 1