Chura-kucha
Chura-kucha wa Afrika (Xenopus laevis)
Chura-kucha wa Afrika (Xenopus laevis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Amphibia (Wanyama wanaoanza maisha kwenye maji na kuendelea nchi kavu)
Nusungeli: Lissamphibia (Amfibia waliopo bado)
Oda: Anura (Vyura)
Nusuoda: Mesobatrachia
Familia: Pipidae (Vyura-kucha)
Ngazi za chini

Jenasi 5:

Vyura-kucha ni aina za vyura ambao wanaishi majini maisha yao yote. Miguu yao ya nyuma ina ngozi katikati ya vidole lakini miguu ya mbele hainayo, isipokuwa vyura-kucha wadogo ambao wana ngozi katikati ya vidole vya miguu yote. Kuna vidole vitano kwa miguu ya nyuma lakini vidole vinne kwa miguu ya mbele. Vidole vitatu vya miguu ya nyuma vina ukucha mweusi. Mwili wao ni mpanapana na ngozi ni ya kuteleza kwa sababu ya ute mwingi. Vyura hawa hawana ulimi. Hufanya sauti kama mialiko kwa mfupa wa hayoidi (hyoid bone).

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za Amerika ya Kusini

hariri
  NODES
os 3