Darubini (kutoka Kiajemi: دوربين, dorbin) ni kifaa cha kutazamia vitu ambavyo viko mbali. Kutegemeana na kusudi lake kuna aina mbalimbali:

Darubini ya mkononi
Darubinilezi kubwa kwenye paoneaanga pa Chuo Kikuu cha Vienna
Darubiniredio yenye kipenyo cha mita 12 pale Kitt Peak, Arizona, USA

Historia ya darubini

hariri

Darubini ya kwanza inayojulikana ilitengenezwa mwaka 1608 na Mholanzi Hans Lipperhey aliyekuwa fundi miwani akaunganisha lenzi mbili katika bomba.

Mfano wake ulichukuliwa na kuboreshwa na mwanaastronomia Mwitalia Galileo Galilei aliyeanza kuitumia mwaka 1610 kwa kuangalia nyota. Aligundua mara moja miezi ya sayari Mshtarii.

Muundo tofauti uligunduliwa na padre Nicolaus Zucchius mwaka 1616 uliotumia kiakisi parabola kwa kukusanya mishale ya nuru.

Katika karne zilizofuata vyombo hivyo viliendelea kuboreshwa.

Mtambo mpya ulipatikana katika karne ya 20 kwa kutumia mnururisho wa sumakuumeme kutoka nyota iliyoendelezwa kuwa darubiniredio.

Elimu ya ulimwengu wetu ilipanuka sana tangu kupelekwa kwa darubini za angani kwenye anga-nje zinazopokea nuru na mawimbi ya sumakuumeme bila athari ya angahewa ya Dunia.

Viungo vya nje

hariri

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  NODES
Done 1