Dvina ya Kaskazini

Dvina ya Kaskazini (kwa Kirusi: Се́верная Двина́) ni mto mkubwa katika kaskazini ya Urusi unaopitia Vologda Oblast na Arkhangelsk Oblast ukiishia katika Hori ya Dvina ya Bahari Nyeupe.

Mto Dvina ya Kaskazini
Ramani ya bonde la Dvina Kaskazini
Day Quay ya Kaskazini huko Arkhangelsk

Matawimto makuu ni Vychegda (kulia), Vaga (kushoto), na Pinega (kulia).

Jiografia

hariri

Urefu wa Dvina ya Kaskazini ni km 774.

Eneo la bonde lake ni km² 357,052.

Miji ya Arkhangelsk na Vologda iko kwenye beseni la Dvina ya Kaskazini, pamoja na miji mingi kidogo. Mingi ina umuhimu wa kihistoria kama vile Veliky Ustyug, Totma, Solvychegodsk, na Kholmogory.

Katika majira ya joto barafu ya miezi mingi inayeyuka na hapo mto hutumiwa kama njia ya kusafirisha mbao wa miti iliyokatwa msituni na kupelekwa penye viwanda vya kuupasulia.

Mnamo 1926-1928 mfereji wa kuunganisha mto Pinega, moja ya matawimto makuu ya Dvina ya Kaskazini, ulijengwa kwa kuuunganisha na mto Kuley, lakini mfereji hauna matumizi sana.[1]

Marejeo

hariri
  1. "Канал рек Пинега-Кулой надо восстановить". Russian Geographic Society (kwa Russian).{{cite web}}: CS1 maint: unrecognized language (link)

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Dvina ya Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES