Gauteng
Gauteng ni moja kati ya majimbo 9 ya Afrika Kusini. Mji mkuu ni Johannesburg. Jimbo lilianzishwa baada ya mwisho wa siasa ya Apartheid kutoka kwa sehemu ya jimbo la Transvaal ya awali. Mwanzoni lilitwa "Pretoria-Witwatersrand-Vereeniging" lakini jina likabadilishwa tena kuwa Gauteng. Neno Gauteng limetokana katika lugha ya Kisotho lamaanisha "mahali pa dhahabu" kwa kukumbuka umuhimu wa migodi ya dhahabu katika eneo la Johannesburg.
Eneo | 17,010 km² |
Wakazi(2001) | 8,837,172 |
Lugha | Kizulu (21.5%) Kiafrikaans (14.4%) Kisotho (13.1%) Kiingereza (12.5%) |
Wakazi kimbari | Waafrika Weusi(73.8%) Wazungu(19.9%) Chotara(3.8%) Wenye asili ya Asia (2.5%) |
Mji Mkuu | Johannesburg |
Waziri Mkuu | Mbhazima Shilowa (ANC) |
Hata kama eneo la jimbo ni 17,000 km² pekee idadi ya watu ni kubwa. Kieneo Gauteng ni jimbo dogo la nchi lakini ina nafasi ya pili kufuatana na idadi ya wakazi; imekadiriwa ya kwamba karibuni Gauteng itapita KwaZulu-Natal na kuwa jumbo lenye watu wengi katika Afrika Kusini.
Gauteng ni kitovu cha uchumi wa taifa. 9% za pato la uchumi wa afrika yote huzalishwa hapa.
Jimbo hili lina mchanganyiko wa makabila yote. Utajiri na umaskini hukaa karibu sana. Kati ya matatizio makubwa ni uhalifu. watu wa Johannesburg wanazidi kufa kutokana na kuuawa kushinda vifo vya barabarani. Inahesabiwa kuwa kati ya mahali penye hatari kabisa duniani.
Miji mingine ya maana ni kama hii:
- Pretoria (sehemu ya manisipaa ya Tshwane)
- Soweto (sehemu ya manisipaa ya City of Johannesburg)
- Heidelberg
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Gauteng kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |