George Washington

Rais wa kwanza wa Marekani

George Washington (22 Februari 1732 - 14 Desemba 1799) alikuwa mwanasiasa, kiongozi wa kijeshi na rais wa kwanza wa Marekani kati ya 1789 na 1797.

George Washington

Rais George Washington, mnamo 1797

Muda wa Utawala
April 30, 1789 – March 4, 1797
Makamu wa Rais John Adams
aliyemfuata John Adams

tarehe ya kuzaliwa (1732-02-22)Februari 22, 1732
tarehe ya kufa 14 Desemba 1799 (umri 67)
Mount Vernon, mjini Virginia
mahali pa kuzikiwa Washington Family Tomb
chama Independent
ndoa Martha Dandridge (m. 1759) «start: (1759-01-06)»"Marriage: Martha Dandridge to George Washington" Location: (linkback://sw.wikipedia.org/wiki/George_Washington)
signature
Washington akisimamia shamba na watumwa.
Washington akivuka mto Delaware katika vita ya uhuru ya Marekani.
Sanamu ya Washington pamoja na maraisi wengine kwenye mlima Rushmore
Nyumba yake kwenye shamba la Mount Vernon
Washington kwenye pesa la Marekani.

Mtoto na kijana

hariri

Alizaliwa kama mtoto wa pili wa mlowezi Augustine Washington katika koloni la Virginia lililokuwa mali ya mfalme wa Uingereza.

Wazazi walikuwa na shamba kubwa lililolimwa na watumwa Waafrika.

George alisoma shule miaka michache, hakuendelea sana katika elimu. Baada ya shule alianza kazi ya upimaji na ramani.

Mkulima na kiongozi wa kijeshi

hariri

Baada ya kifo cha kaka yake alirithi shamba kubwa pamoja na watumwa, akawa mkulima tajiri. Sehemu ya urithi ilikuwa cheo cha msimamizi wa wanamgambo waliokuwa kikosi cha kijeshi cha hiari waliotakiwa kusaidiana na wanajeshi Waingereza kutetea koloni dhidi ya majirani Waindio na Wafaransa walioenea kuelekea kusini kutoka koloni lao la Kanada - Quebec.

Katika umri mdogo wa miaka 22 Washington alijikuta kama mkuu wa wanamgambo katika vita vya Uingereza dhidi ya Wafaransa na Waindio vilivyopanuka baadaye kuwa Vita ya Miaka Saba. Akaongoza kikosi chake dhidi ya maadui akafaulu mara kadhaa.

Baadaye alishirikiana na jeshi rasmi la Uingereza katika mapigano ya Monongahela na kuongoza mabaki ya jeshi baada ya kifo cha jemadari Mwingereza. Mwaka 1755 akawa mkuu wa jeshi la koloni la Virginia. Lakini baada ya ushindi Waingereza walikataa kumpa cheo katika jeshi la mfalme, hivyo akajiuzulu akarudi kwenye shamba lake na kufuata siasa kwenye bunge la koloni.

Mwaka 1759 Washington akaoa mjane tajiri akawa kati ya matajiri wakuu kabisa wa Virginia.

Mapinduzi

hariri

Baada ya vita ya miaka saba uhusiano kati ya Uingereza na walowezi Waingereza katika makoloni yake 13 ya Amerika ya Kaskazini ukazorota. Tangu mwaka 1773 Waingereza walitumia sheria ya dharura na nguvu ya kijeshi mjini Boston. Wawakilishi wa makoloni yote 13 wakakutana kama bunge la Amerika Bara na Washington alikuwa miongoni mwao.

Baada ya mapigano ya kwanza kati ya wanajeshi Waingereza na wanamgambo wa walowezi, bunge likaamua kuunda jeshi la pamoja la makoloni yote na Washington akateuliwa kuwa jemadari mkuu.

Aliongoza jeshi la Marekani katika vita ya uhuru wa Marekani dhidi ya Uingereza hadi mwaka 1783.

Baada ya vita: mwanasiasa na rais

hariri

Baada ya uhuru wa Marekani George Washington akarudi kwake akalima tena lakini akachaguliwa pia kama mwakilishi wa Virginia katika bunge la katiba la Marekani mwaka 1787 akawa mwenyekiti wa mkutano huu uliokubali katiba ya Marekani.

Tarehe 4 Februari 1789 alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Marekani akirudishwa mwaka 1789. Baada ya kipindi chake cha pili alikataa kusimama tena akaunda hivyo utaratibu wa kwamba rais anaweza kurudishwa mara moja tu, hawezi kuendelea zaidi.

Mwisho na heshima baada ya kifo

hariri

Mwaka 1797 akarudi tena kwake shambani aliposimamia kilimo kilichoendeshwa na watumwa 390. Tarehe 14 Desemba 1799 alikufa kwake nyumbani. Kabla ya kuaga dunia aliamuru katika usia wake ya kwamba watumwa wake wote wapewe uhuru baada ya kifo chake yeye mwenyewe na mke wake.

Mji mkuu wa Marekani Washington, D.C. na jimbo la Washington vimepokea majina kutokana naye.

Picha yake iko kwenye noti ya dollar moja.

}}

  NODES