Helikopta ni aina ya chombo cha usafiri wa anga ambacho hakina mabawa yaliyofungwa imara, ila mikono ya rafadha iliyopo wima juu ya chombo inayofanya kazi ya mabawa ya ndege yakizunguka haraka na kusababisha kani ya mnyanyuo (en:lift (force)} inayoiinua. Hayo yanakiwezesha kuinuka na kutua wima mahali popote, kwenda mbele au kurudi nyuma, kuelea angani na hata kujongea kiupandeupande.

Helikopta 1922
Hii ni helikopta ya kuzima moto.
Hii ni helikopta ya vita.

Tabia hizo zinaruhusu helikopta kutumika katika maeneo yaliyojaa au yaliyotengwa ambapo ndege haziwezi kufanya kazi kutokana na jinsi ilivyoundwa.

Kuna aina mbalimbali za helikopta kama helikopta za uzimaji moto, za vita n.k.

Jina helikopta hutoka katika neno la Kiingereza "helicopter" ambalo limetoholewa kutoka neno la Kifaransa "helicoptere" lililotajwa na Gustave Ponton d'Amécourt mnamo mwaka 1861, ambayo asili yake ni katika maneno ya Kigiriki helix (ἕλιξ) lenye maana ya "izungukayo" na pteron (πτερόν) lenye maana ya "mbawa".

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
Done 1
see 1