Ionia ilikuwa eneo la kihistoria katika magharibi ya Asia Ndogo zamani za Ugiriki ya Kale. Leo hii eneo lake liko ndani ya Uturuki.

Mahali pa Ionia katika Uturuki wa leo
Kichwa cha nguzo katika mtindo wa Kiionia
Mtindo wa Kiionia kwenye jengo la bima huko Cicinnati (Marekani) mnamo mwaka 1900 BK

Jina la Ionia lilitokana na Waionia waliokuwa kabila la Wagiriki waliohamia Asia Ndogo kutoka Ugiriki mwenyewe mnamo mwaka 1,000 KK na kujenga miji yao huko kama vile Efeso, Mileti na Smirna (Izmir ya leo). Baadaye Ionia ilikuwa eneo walipoishi wanafalsafa muhimu kama Thales wa Mileti, Anaximander oder Heraklito.

Ionia ilikuwa pia na wasanii bora hasa mtindo wa nguzo wa Kiionia umepata maarufu ukarudiwa pia katika majengo ya kisasa.

Neno "Ionia" ni asili kwa jina la "Yunan" (یونان) katika Kiarabu au "Yunani" katika Kiswahili cha zamani kwa ajili ya nchi ya Ugiriki au "Kiyunani" kwa ajili ya lugha ya Kigiriki.

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.


  NODES