Jamhuri ya Masedonia Kaskazini

(Elekezwa kutoka Jamhuri ya Masedonia)

Jamhuri ya Masedonia Kaskazini (jina jipya lililoanza kutumika mnamo Februari 2019; kwa Kimasedonia: Република Северна Македонија, Republika Severna Makedonija; kwa Kialbania: Republika e Maqedonisë së Veriut) ni nchi kwenye rasi ya Balkani katika Ulaya ya kusini mashariki. Imepakana na Serbia, Albania, Ugiriki na Bulgaria.

Република Северна Македонија
Republika e Maqedonisë së Veriut

Jamhuri ya Masedonia Kaskazini
Bendera ya Masedonia Kaskazini Nembo ya Masedonia Kaskazini
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: {{{national_motto}}}
Wimbo wa taifa: Денес над Македонија
Leo juu ya Masedonia
Lokeshen ya Masedonia Kaskazini
Mji mkuu Skopje (tamka: "skopye"
42°0′ N 21°26′ E
Mji mkubwa nchini Skopje
Lugha rasmi Kimasedonia1
Serikali Jamhuri ya kibunge
Gordana Siljanovska-Davkova (Гордана Сиљановска-Давкова)
Hristijan Mickoski (Христијан Мицкоски)
Independence
Ilitangazwa
8 Septemba 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
25,333 km² (ya 148)
1.9
Idadi ya watu
 - 2011 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
2,058,539 (ya 146)
80.1/km² (ya 122)
Fedha Denar ya Masedonia (MKD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .mk
Kodi ya simu +389

-

1Kimasedonia ndiyo lugha rasmi pamoja na Kialbania. Kila lugha inayotumiwa na 20% ya wakazi hutumiwa kama lugha rasmi ya nyongeza kimahali kama vile Kituruki, Kiromany na Kiserbia.


Ramani ya Jamhuri ya Masedonia Kaskazini.

Mji mkuu ni Skopje, wenye wakazi 600,000. Miji midogo zaidi ni pamoja na Bitola, Prilep, Tetovo, Kumanovo, Ohrid, Veles, Štip, Gostivar na Strumica.

Masedonia Kaskazini ni nchi mwanachama ya Umoja wa Mataifa na inasubiri kupokewa katika Umoja wa Ulaya.

Historia

hariri

Masedonia ya Kale

hariri

Katika karne za kabla ya Kristo Masedonia ilikuwa eneo la kaskazini la Ugiriki. Wakazi wake wanaaminiwa walisema lahaja za Kigiriki, lakini mara nyingi hawakutambuliwa na Wagiriki wenyewe kama wenzao, jinsi tunavyojua kutoka waandishi wa Ugiriki ya Kale.

Mnamo 500 KK kulikuwako ufalme ulioitwa Masedonia na wafalme waliruhusiwa kwenye michezo ya Olimpiki ya madola ya Wagiriki.

Pamoja na sehemu nyingi za Ugiriki ufalme huo ulipaswa kukubali ubwana wa Milki ya Uajemi, lakini mfalme Filipo II wa Masedonia alifaulu, kuanzia mnamo mwaka 360 KK, kurudisha uhuru wa ufalme akaendelea kuifanya Masedonia kuwa dola kiongozi kati ya madola madogo ya Ugiriki.

Mwanawe Aleksander aliimarisha utawala wake juu ya Wagiriki wengine na kushambulia Milki ya Uajemi na hatimaye kuivamia na kuishinda kwa jeshi la Wagiriki kutoka sehemu zote.

Mnamo mwaka 325 KK mfalme wa Masedonia alitawala nchi zote kuanzia Ugiriki hadi Misri, Syria, Uajemi, mipaka ya Uhindi na Asia ya Kati.

Baada ya kifo cha Aleksander mnamo 323 KK milki yake iligawiwa, na Masedonia ilikuwa tena ufalme wa pekee. Ikaendelea kwa kujitegema hadi uenezi wa Dola la Roma ikawa jimbo la Kiroma tangu mwaka 147 KK.

Baadaye ufalme wa awali iligawiwa kwa majimbo mbalimbali. Wakazi walibadilika polepole kutokana na uhamiaji ndani ya Dola la Roma.

Kufika kwa Waslavi

hariri

Tangu karne ya 6 BK makabila ya Waslavi yalifika katika sehemu zilizowahi kuitwa Masedonia zamani. Sehemu kubwa ya eneo ilikuwa chini ya milki ya Wabulgaria, tangu 1018 sehemu ya jimbo la Bulgaria katika Milki ya Bizanti.

Mnamo 1392 Waturuki Waosmani walianza kuvamia Masedonia iliyoendelea kukaa chini ya Milki ya Osmani hadi 1912.

Masedonia ya sasa

hariri

Sehemu kubwa ya Masedonia ya Kale leo hii iko ndani ya Ugiriki na pia Bulgaria. Jamhuri ya leo ina tabia ya pekee kwa sababu ilikuwa sehemu ya Yugoslavia hadi 1991.

Masedonia ni eneo linalokaliwa hasa na Waslavoni wanaozungumzwa lugha iliyo karibu na Kibulgaria na pia Kiserbia. Eneo hili lilitawaliwa kwa muda mrefu na Dola la Uturuki. Si rahisi kujua watu wa sehemu hizi walianza lini kujisikia kama watu tofauti na wa pekee na majirani yao hasa Wabulgaria. Inaonekana hii ilitokea hasa wakati wa karne ya 20.

Masedonia ya leo ilikuwa jimbo la kujitawala la Yugoslavia. Baada ya mwisho wa shirikisho la Yugoslavia, Masedonia nayo ilitafuta uhuru wake.

Mwanzoni palikuwa na matatizo ya kutumia jina hilo kwa sababu ya upinzani wa Bulgaria na Ugiriki zinazodai kuwa "Masedonia" ni sehemu ya urithi wao wa kitaifa. Kwa muda nchi ilijulikana rasmi kama "Masedonia iliyokuwa jamhuri ya Yugoslavia" lakini yenyewe iliamua kujiita "Jamhuri ya Masedonia" tu.

Wakazi na utamaduni

hariri

Wamasedonia Waslavoni ni takriban theluthi mbili za wakazi wote. Robo moja ni Waalbania. Wengine ni mchanganyiko wa vikundi vidogovidogo kama Waturuki, Waromany na Waserbia.

Lugha rasmi ni Kimasedonia, lakini kwa kiasi fulani Kialbania pia, mbali ya lugha za kieneo.

Wamasedonia wenyewe ni hasa Wakristo Waorthodoksi (64.7% za wakazi wote). Waalbania na Waturuki ni hasa Waislamu (33.3%). Lakini zaidi ya theluthi ya watu wote husema ya kwamba hawana dini. Hii inaaminiwa ni urithi wa kipindi cha ukomunisti nchini.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jamhuri ya Masedonia Kaskazini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
Intern 1
mac 7
os 12
web 1