Kalenda ya Ethiopia
Kalenda ya Ethiopia (kwa Kiamhari: የኢትዮጵያ ዘመን አቆጣጠር ye'Ityoṗṗya zemen aḳoṭaṭer) ni kalenda rasmi nchini Ethiopia na pia kalenda inayotumiwa na Wakristo walio wengi nchini Eritrea. Asili yake ni kalenda ya Wakopti kwa sababu Kanisa la Ethiopia kwa karne nyingi lilikuwa kama tawi la kanisa la Kikopti la Misri.
Miezi 13 na miaka mirefu
haririKalenda huwa na mwaka wa miezi 13; miezi kamili 12 ya siku 30 na mwezi wa 13 mfupi wa siku 5 yaani jumla siku 365. Kila mwaka wa 4 ni mwaka mrefu ambako mwezi wa 13 huwa na siku 6 yaani siku 366 kwa jumla. Chanzo cha mwaka kinalingana na 11 Septemba ya kalenda ya Gregori (kalenda ya kimataifa), isipokuwa baada ya mwaka mrefu kinalingana na 12 Septemba na tofauti inasawazishwa katika mwaka mrefu wa kalenda ya Gregori.
Tofauti na kalenda ya Gregori utaratibu wa mwaka mrefu kila mwaka wa nne unaendelea bila kituo.
Hesabu ya miaka
haririHesabu ya miaka ni tofauti na mwaka wa Gregori kiasi cha miaka 7-8. Sababu yake ni ykwamba kalenda hii, sawa na ya Wakopti, hufuata makadirio ya mwaka wa kuzaliwa kwake Yesu ambayo ni tofauti kidogo na hesabu ya magharibi inayomfuata Dionysius Exiguus. Kati ya Januari hadi 10/11 Septemba tofauti ni miaka 8, kwa miezi inayobaki tofauti ni miaka 7. Kwa hiyo mwaka 2007 ya kalenda ya kimataifa ililingana na mwaka 2000 wa Ethiopia.
Miezi
haririGe'ez, Kiamhari na Kitigrinya | Kikopti | Chanzo cha mwaka katika kalenda ya Gregori |
Chanzo cha mwaka baada ya mwaka mrefu |
---|---|---|---|
Mäskäräm (መስከረም) | Tut | 11 Septemba | 12 Septemba |
Ṭəqəmt(i) (ጥቅምት) | Babah | 11 Oktoba | 12 Oktoba |
Ḫədar (ኅዳር) | Hatur | 10 Novemba | 11 Novemba |
Taḫśaś ( ታኅሣሥ) | Kiyahk | 10 Desemba | 11 Desemba |
Ṭərr(i) (ጥር) | Tubah | 9 Januari | 10 Januari |
Yäkatit (Tn. Läkatit) (የካቲት) | Amshir | 8 Februari | 9 Februari |
Mägabit (መጋቢት) | Baramhat | 10 Machi | 10 Machi |
Miyazya (ሚያዝያ) | Baramundah | 9 Aprili | 9 Aprili |
Gənbot (ግንቦት) | Bashans | 9 Mei | 9 Mei |
Säne (ሰኔ) | Ba'unah | 8 Juni | 8 Juni |
Ḥamle (ሐምሌ) | Abib | 8 Julai | 8 Julai |
Nähase (ነሐሴ) | Misra | 7 Agosti | 7 Agosti |
Ṗagʷəmen/Ṗagumen (ጳጐሜን/ጳጉሜን) | Nasi | 6 Septemba | 6 Septemba |
Marejeo
hariri- "The Ethiopian Calendar", Appendix IV, C.F. Beckingham and G.W.B. Huntingford, The Prester John of the Indies (Cambridge: Hakluyt Society, 1961).
- Ginzel, Friedrich Karl, "Handbuch der matematischen und technischen Chronologie", Leipzig, 3 vol., 1906-1914
Viungo vya Nje
hariri- The Ethiopian Time and Date Online converter with links to free Yahoo widget and iPhone app
- The Ethiopic Calendar by Aberra Molla Archived 5 Septemba 2007 at the Wayback Machine.
- Ethiopian Calendar Converter Archived 12 Mei 2015 at the Wayback Machine.
- Ethiopian Perpetual Calendar Software
- Ethiopian Online Calendar Archived 18 Septemba 2007 at the Wayback Machine.
- Siyan Gregorian-Ethiopic Date converter applet Archived 14 Machi 2012 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kalenda ya Ethiopia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |