Kaunti ya Kwale
Kaunti ya Kwale ni Kaunti nchini Kenya iliyoko kwenye eneo la Mkoa wa Pwani la awali. Mji mkuu uko Kwale lakini mji wake mkubwa ni Ukunda.
Kaunti ya Kwale | |
---|---|
Kaunti | |
Kwale County in Kenya.svg Kaunti ya Kwale katika Kenya | |
Coordinates: 4°10′S 39°27′E / 4.167°S 39.450°E | |
Nchi | Kenya |
Namba | 2 |
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi, 2013 |
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Pwani |
Makao Makuu | Kwale |
Miji mingine | Ukunda, Mariakani, Msambweni, Lunga Lunga |
Gavana | Salim Mvurya |
Naibu wa Gavana | Fatuma Mohamed Achani |
Seneta | Issa Juma Boy |
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Zuleikha Juma Hassan |
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya kwale |
Spika | Sammy Ruwa |
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 4 |
Eneo | km2 8 267.1 (sq mi 3 191.9) |
Idadi ya watu | 866,820 |
Wiani wa idadi ya watu | 105 |
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) |
Tovuti | kwalecountygov.com |
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 eneo la kaunti lilikuwa na wakazi 866,820 katika eneo la km2 8,267.1, msongamano ukiwa hivyo wa 105 kwa kilometa mraba[1].
Kwale ina sehemu ya pwani kwenye mwambao wa Bahari Hindi kati ya Mombasa na Tanzania. Sehemu zinazotembelea sana na watalii ni Diani Beach katika tarafa ya Msambweni, Shimba Hills National Reserve na Patakatifu pa tembo pa Mwaluganje.
Utawala
haririKaunti ya Kwale ina maeneo bunge yafuatayo[2][3]:
Eneo Bunge | Kata |
---|---|
Msambweni | Gombato Bongwe, Ukunda, Kinondo, Ramisi |
Lunga Lunga | Pongwe / Kikoneni, Dzombo, Mwereni, Vanga |
Matuga | Tsimba Golini, Waa, Tiwi, Kubo Kusini, Mkongani |
Kinango | Ndavaya, Puma, Kinango, Mackinnon Road, Chengoni / Samburu, Mwavumbo, Kasemeni |
- Kinango 94,220
- Lunga Lunga 198,423
- Matuga 194,252
- Msambweni 177,690
- Samburu-Kwale 202,235
Miji
haririTazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ www.knbs.or.ke
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-09-04. Iliwekwa mnamo 2021-09-04.
- ↑ "Wawakilishi wa Wadi katika bunge la Kwale Ilihifadhiwa 24 Septemba 2014 kwenye Wayback Machine.", Serikali ya Kaunti ya Kwale, ilipatikana 08-04-2018
- ↑ www.knbs.or.ke
Viungo vya Nje
hariri- http://www.mambolook.com/kwale Ilihifadhiwa 30 Juni 2017 kwenye Wayback Machine. Ilihifadhiwa 30 Juni 2017 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kaunti ya Kwale kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |