Kaunti ya Makueni
Kaunti ya Makueni ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Kaunti ya Makueni | |
---|---|
Kaunti | |
Haven of Opportunities | |
Makueni County in Kenya.svg Kaunti ya Makueni katika Kenya | |
Coordinates: 1°48′S 37°37′E / 1.800°S 37.617°E | |
Nchi | Kenya |
Namba | 17 |
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi, 2013 |
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Mashariki |
Makao Makuu | Wote |
Miji mingine | Emali, Makindu, Kibwezi, Mtito Andei |
Gavana | Prof. Kivutha Kibwana, EGH |
Naibu wa Gavana | Adelina Mwau Ndeto, OGW |
Seneta | Mutula Kilonzo Junior |
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Rose Mumo |
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya Makueni |
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa | 30 |
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 6 |
Eneo | km2 8 169.8 (sq mi 3 154.4) |
Idadi ya watu | 987,653 |
Wiani wa idadi ya watu | 121 |
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) |
Tovuti | makueni.go.ke |
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 987,653 katika eneo la km2 8,169.8, msongamano ukiwa hivyo wa watu 121 kwa kilometa mraba[1].
Makao makuu yako Wote.
Jiografia
haririKaunti ya Makueni imepakana na Machakos (kaskazini), Kitui (mashariki), Taita Taveta (kusini) na Kajiado (magaribi). Ni kaunti nusu kavu. Tabianchi hii huiwezesha Makueni kuzalisha maembe kwa muda mrefu kwa mwaka.
Mto Athi hupitia katika mpaka wa mashariki. Kulingana na utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta, asilimia 39 ya Makueni ina maji chini ya ardhi[2].
Tambarare ya Yatta huwa katika kaskazini mwa kaunti. Vilima vya Chyulu na Mbuga ya Kitaifa ya Vilima vya Chyulu huwa kusini mwa kaunti.
Utawala
haririKaunti ya Makueni imegawanywa katika maeneo bunge yafuatayo[3]:
- Kathonzweni 79,780
- Kibwezi 197,000
- Kilungu 60,952
- Makindu 84,946
- Makueni 130,375
- Mbooni East 97,756
- Mbooni West 102,594
- Mukaa 107,549
- Nzaui 126,701
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
- ↑ "Hope in Tapping Underground Water in Makueni - Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-02. Iliwekwa mnamo 2018-04-26.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-09-04. Iliwekwa mnamo 2021-09-04.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kaunti ya Makueni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |