Kiakisi parabola (kwa Kiingereza: parabolic reflector, pia kioo parabola parabolic mirror) ni uso wa gimba wenye umbo la parabola. Hutumiwa kukusanya au kuvurumisha nishati kama vile nuru, sauti au wimbiredio.

Kiakisi parabola katika antena ya mawasiliano na satelaiti

Mawimbi yanayoingia katika eneo la kiakisi parabola hukusanywa kwenye fokasi yake. Kwa hiyo kinafaa kama kipokezi cha mawimbi sumakuumeme yanayotoka kwenye umbali mkubwa kama nyota. Kinyume chake kiakisi parabola kinaweza kukusanya miale ya rada au kutumiwa kwenye taa, kwa mfano taa ya gari. Zinafaa pia kupaza sauti.

Kwa matumizi na mawimbi ya nuru kiakisi parabola hutengenezwa kwa kutumia kioo (pia kauri) kinachopokea umbo lake kwa kukisaga. Darubini kubwa za astronomia hutumia mfumo huo. Kwa wimbiredio kiakisi hutengenezwa kwa kawaida kwa kutumia metali. Sahani ya satelaiti inayotumiwa kupokea programu za runinga huwa na umbo la kiakisi parabola.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES