Kwa matumizi mengine ya jina hili tazama Kilwa


Kilwa Kivinje
Nchi Tanzania
Mkoa Lindi
Wilaya Kilwa
Muonekano wa Boma la Ujerumani huko Kilwa karne ya 19

Kilwa Kivinje ni mji mdogo katika Wilaya ya Kilwa ufukoni wa Bahari Hindi. Kiutawala ni sehemu ya kata ya Kivinje Singino.

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, mji ulilikuwa na wakazi wapatao 15,061. Msimbo wa posta ni 65402.

Historia

hariri

Wakati wa utawala wa Zanzibar ilikuwa makao ya liwali ya Sultani kwa ajili ya pwani la kusini la Tanganyika ikichukua nafasi ya Kilwa Kisiwani kama bandari muhimu katika sehemu hii ya pwani la kusini. Kivinje ilikuwa lengo la misafara ya watumwa katika kusini ya Tanzania. the mainland port of Kilwa Kivinje supplanted Kisiwani as the terminus of the southern slave caravan. Bandari yake ya mchanga ilifaa kwa maboti madogo ya ubao waliobeba watumwa Zanzibar. Kuna makadirio ya kwamba watumwa 20,000 walipita Kivinje kila mwaka.[1] Mnamo mwaka 1850 Kivinje ilikuwa mji wa wakazi 12-15,000 pamoja na wanfanyabiashara wenye asili ya Uhindini. Baada ya Sultani wa zanzibar kupiga biashara ya watumwa marufuku Kivinje ilijulikana kwa kuendelea na biashara hii kwa siri. Zanzibar ilimkamata sulatani wa mwisho wa Kivinje na kumtuma nje ya mji.[2]

Ilikuwa makao makuu ya wilaya tangu zamani ya ukoloni wa Kijerumani. Wakati wa vita ya Abushiri iliona mapigano dhidi ya Wajerumani na wawakilishi wa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki waliuawa tar. 22 Septemba 1888. Mei 1890 Wajerumani walirudi chini ya meja Hermann von Wissmann wakateka mji bila upinzani.

Wakati wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani Kilwa Kivinje ilikuwa makao makuu ya mkoa wa nane iliyoenea kati ya Rufiji na Lindi. Utawala wa Kijerumani kilikwisha tar. 7 Septemba 1916 siku ambako Wajerumani waliobaki mjini walijisalimisha mbele ya kikosi cha wanamaji Waingereza.

Mji uliendelea kuwa makao makuu ya wilaya chini ya Waingereza.

Hali ya mji leo

hariri

Tangu kuondoka kwa makao makuu ya wilaya mji umerudi nyuma. Nyumba za ghorofa za wafanyabiashara hazitumiki tena zimeanza kuporomoka. Boma la Kale la Wajerumani bado linatumika.

Hospitali ya wilaya imebaki Kilwa Kivinje. Bandari ndogo inafaa kwa jahazi tu.

Eneo la kihistoria lina magofu ya majengo ya Waswahili ya enzi za kati na baadhi ya majengo ya kiswahili yaliyosalia kutoka mwishoni mwa karne ya 19. [3] Makazi haya yanachukuliwa kama kimbilio la wenyeji wa awali kutoka Kilwa Kisiwani ambao walikuwa wakimbizi kutoka kwa Vasco da Gama ambae alikuwa akiwafukuza mji huo mnamo 1505 na pia kuwachukua kama wakimbizi waliokimbia maharamia wa Madagaska mnamo 1822. [4]

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Kuhusu Kilwa pamoja na Kivinje, kwenye tovuti ya expertafrica.com, ilitazamiwa Juni 2016
  2. Kilwa District - History Ilihifadhiwa 8 Agosti 2016 kwenye Wayback Machine. kwenye tovuti ya Mpingo Conservation and Development Initiative, ilitazamiwa Juni 2016
  3. Chittick, H. Neville (1969,01,01). "The early history of Kilwa Kivinje" (kwa English). {{cite journal}}: Check date values in: |date= (help); Cite journal requires |journal= (help)CS1 maint: unrecognized language (link)
  4. https://journals.udsm.ac.tz/index.php/sap/article/viewFile/2758/2806

Viungo vya nje

hariri
  Kata za Wilaya ya Kilwa - Mkoa wa Lindi - Tanzania  

Chumo | Kandawale | Kibata | Kikole | Kinjumbi | Kipatimu | Kiranjeranje | Kivinje | Lihimalyao | Likawage | Mandawa | Masoko | Miguruwe | Mingumbi | Miteja | Mitole | Namayuni | Nanjirinji | Njinjo | Pande | Somanga | Songosongo | Tingi


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Lindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kilwa Kivinje kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.
  NODES