Kisumu
Kisumu ni mji mkubwa wa tatu wa Kenya, ukiwa na wakazi 968,909 (sensa ya mwaka 2009[1]). Pia ni mji mkubwa wa Kenya ya Magharibi na makao makuu ya kaunti ya Kisumu.
Kisumu | |
Mahali pa mji wa Kisumu katika Kenya |
|
Majiranukta: 0°6′0″S 34°45′0″E / 0.10000°S 34.75000°E | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Kaunti | |
Kisumu | |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 968,909 |
Mji uko kando ya ziwa Viktoria Nyanza, una bandari kubwa ya nchi katika ziwa hilo. Mji na bandari vilianzishwa kwa jina la "Port Florence" mwaka 1901 wakati reli ya Uganda ilipofika huko kutoka Mombasa.
Kuna feri ziwani kutoka Kisumu kwenda Mwanza, Bukoba, Entebbe, Port Bell na Jinja.
Kiuchumi Kisumu ina viwanda kadhaa, hasa vya sukari, samaki, vitambaa, pia ya bia.
Maendeleo ya Kisumu yalikwama miaka mingi kwa sababu kwa miaka mingi Wajaluo walisimama upande wa upinzani wa kisiasa, hivyo serikali haikupeleka miradi tena katika eneo hilo.
Tazama pia
Tanbihi
- ↑ Sensa ya Kenya 2009 Ilihifadhiwa 9 Januari 2019 kwenye Wayback Machine., tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kisumu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |