Kitabu cha Mhubiri

wa ishirini ya kwanza kitabu Biblia, mchanganyiko 12 sura ya

Mhubiri (pia: Koheleti, ing. Ecclesiastes) ni kimojawapo kati ya vitabu vya hekima vilivyomo katika Tanakh (Biblia ya Kiebrania) na hivyo pia katika Agano la Kale la Biblia ya Kikristo. Kwa sababu hiyo kilidhaniwa kimeandikwa na mfalme Solomoni, kielelezo cha hekima katika Biblia.

Kitabu hicho kina sura kumi na mbili na kwa kiasi kikubwa kimeandikwa kwa njia ya ushairi.

Katika lugha ya Kiebrania jina lake ni קֹהֶלֶת (Qohelet), maana yake "Mhadhiri": ndivyo anavyojiita mwandishi, ambaye hajulikani kwa jina.

Yeye anakabili masuala ya maisha kwa kuzingatia upande chanya na upande hasi wa kila moja ili kufikia hekima.

Hasa anajiuliza juu ya maana ya maadili wakati ufunuo wa Mungu ulikuwa haujafikia hatua ya kufundisha uzima wa milele na maisha yalikuwa yanaonyesha mara nyingi ustawi wa waovu na hali ngumu ya waadilifu.

Mbele ya utovu wa haki duniani, Mhubiri alikariri, "Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili" (1:2).

Hata hivyo, hatimaye akajumlisha mawazo yake kwa kuhimiza kwa imani, "Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya" (12:13-14).

Ufafanuzi

hariri

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Maendeleo hayo yataweka wazi kwamba hukumu itafanyika baada ya kifo, na kwamba tuzo na [[]]adhabu vitatolewa kwa haki katika uzima wa milele.

Tanbihi

hariri

Marejeo

hariri
  • Bartholomew, Craig (2009). Ecclesiastes. Baker Academic Press. ISBN 9780801026911. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Brettler, Mark Zvi (2007). "The Poetical and Wisdom Books". Katika Coogan, Michael D. (mhr.). The New Oxford Annotated Bible (3rd ed.). Oxford University Press. ISBN 9780195288803. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Brown, William P. (2011). Ecclesiastes: Interpretation: A Bible Commentary for Teaching and Preaching. Westminster John Knox Press. ISBN 9780664238247. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Christianson, Eric S. (2007). Ecclesiastes Through the Centuries. Wiley-Blackwell. ISBN 9780631225294. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Coogan, Michael D. (2008). The Old Testament: A Very Short Introduction. Oxford University Press. ISBN 9780199719464. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Diderot, Denis (1752). Canon. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Eaton, Michael (2009). Ecclesiastes. IVP Academic. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2018-10-26. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help); Unknown parameter |= ignored (help)
  • Enns, Peter (2011). Ecclesiastes. Eerdmans. ISBN 9780802866493. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Fredricks, D.C. (2010). Ecclesiastes and Song of Songs. IVP Academic. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2018-10-26. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help); Unknown parameter |= ignored (help)
  • Fox, Michael V. (2004). The JPS Bible Commentary: Ecclesiastes. Jewish Publication Society. ISBN 9780827609655. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Gilbert, Christopher (2009). A Complete Introduction to the Bible: A Literary and Historical Introduction to the Bible. Paulist Press. ISBN 9780809145522. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Hecht, Jennifer Michael (2003). Doubt: A History. New York: HarperCollins. ISBN 978-0-06-009795-0.

Marejeo mengine

hariri
  • Ranston, Harry (1925). Ecclesiastes and the Early Greek Wisdom Literature. First ed. Epworth Press.
  • Shapiro, Rabbi Rami Translation & Annotation, Foreword by Rev. Barbara Cawthrone Crafton (2010). Ecclesiastes Annotated & Explained. Skylight Paths Publishing

Viungo vya nje

hariri
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Tafsiri za Kiingereza
Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Mhubiri kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES