Kizazi ni kundi la watu waliozaliwa takriban wakati wa pamoja na waliokuwa watoto na vijana pamoja. Dhana hiyo inafanana kiasi fulani na "rika" katika jamii za Kiafrika lakini haitegemei sherehe za pamoja jinsi ilivyo katika rika.

Vizazi vinne vya wakinamama katika familia moja

Kwa lugha nyingine kizazi ni pia watu ndani ya familia au ukoo ambao wamekuwa wazazi takriban wakati moja kwa kutofautisha na kizazi cha mababu waliotangulia au kizazi cha viijana kinachofuata.

Kutokana na matumizi haya neno latumiwa pia kwa kutaja kipindi cha miaka kadhaa, mara nyingi miaka 20 au 25.

  NODES