Kundi la spektra (kwa Kiingereza: spectral class, spectral type) ni namna ya kutaja idadi ya nyota zenye tabia za kifizikia za pamoja jinsi zinavyoonekana katika uchambuzi wa spektra ya nuru zake.

Nyota jinsi zinavyopatikana katika makundi ya spektra.

Mwanga wa nyota unapitishwa katika mche maonzi (prism) unapopindika na kutoka kama kanda la rangi mbalimbali zilizomo ndani yake pamoja na mistari myeusi ya ufyonzaji na mistari myeupe ya utoaji. Kila mstari hudokeza kuwepo kwa elementi za kikemia ilhali upana wa mstari unadokeza wingi wa elementi hiyo.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kundi la spektra kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES