Afrika ya Kusini
(Elekezwa kutoka Kusini mwa Afrika)
Afrika ya Kusini ni ukanda ulioko kusini mwa bara la Afrika.
Katika hesabu ya UM nchi 5 zifuatazo huhesabiwa kuwa sehemu za ukanda huo:
Jina la nchi au eneo, bendera |
Mji Mkuu |
---|---|
Botswana | Gaborone |
Eswatini | Mbabane |
Lesotho | Maseru |
Namibia | Windhoek |
Afrika Kusini | Bloemfontein, Cape Town, Pretoria |
Mara nyingi nchi zifuatazo zinatajwa pia kuwa nchi za Afrika ya Kusini:
- Angola – wakati mwingine kanda la Afrika ya Kati katika orodha ya UM.
- Msumbiji na Madagaska – menginevyo kanda la Afrika ya Mashariki katika orodha ya UM.
- Malawi, Zambia na Zimbabwe – wakati mwingine zinehesabiwa kuwa sehemu ya Afrika ya Kusini au ya Afrika ya Mashariki - (zamani zilikuwa pamoja kama Rhodesia ya Kusini, Rhodesia ya Kaskazini na Unyasa katika Shirikisho la Afrika ya Kati)
- Komori, Morisi, Shelisheli, Mayotte na Réunion ni visiwa vidogo vya Bahari Hindi vinavyohesabiwa kuwa sehemu za Afrika ya Mashariki.