Liturujia ya Canterbury
Liturujia ya Canterbury ni madhehebu yanayoendeleza mambo bora ya Anglikana ndani ya Kanisa la Kilatini.
Mwaka 2011 na 2012 Papa Benedikto XVI alianzisha majimbo matatu kwa Waanglikana walioamua kujiunga na Kanisa Katoliki kama makundi.
La kwanza lilianzishwa kwa wale wa Uingereza na Wales (lakini pia Uskoti), la pili kwa wale wa Marekani (baadaye liliongezewa wale wa Kanada)[1][2], la tatu kwa wale wa Australia (halafu pia Japani). Jumla ya waamini ni 10,000 hivi, chini ya mapadri 190, wengi wao wakiwa na ndoa.
Kila mojawapo linaongozwa na padri mwenye ndoa aliyewahi kuwa askofu wa Kianglikana, isipokuwa lile la Marekani ambalo limepewa askofu wa kwanza ambaye ni mseja.
Kabla ya hapo kulikuwa na parokia tu za namna hiyo huko Marekani na Kanada, zikifuata hati maalumu ya Papa Yohane Paulo II ya tarehe 20 Juni 1980,[3][4][5]
Tarehe 9 Desemba 2009, Benedikto XVI alitoa hati Anglicanorum Coetibus, iliyoweka taratibu za uanzishaji wa majimbo yasiyopakana na majimbo ya kawaida ya Kilatini kwa Wakristo wa namna hiyo[6], na kufikia mwisho wa mwaka 2015 parokia zote zilizoanzishwa kabla ya hapo isipokuwa 2 zimejiunga na jimbo la Kimarekani. Mkutano maalumu kwa ajili hiyo ulifanyika tarehe 8-10 Novemba 2012[7].
Kwa niaba ya Papa, Idara ya Ibada ya Kimungu ilipitisha the Book of Divine Worship kwanza kwa muda mwaka 1984, halafu moja kwa moja mwaka 1987.[4] Kuanzia tarehe 29 Novemba 2015 nafasi yake imeshikwa na "Divine Worship: The Missal".
Ibada nyingine kwa ajili ya ndoa na mazishi zilipitishwa na idara hiyo tarehe 22 Juni 2012[8].
Tanbihi
hariri- ↑ Cardinal Levada, William (1 Januari 2012). "Decree of Erection of the Personal Ordinariate of the Chair of Saint Peter" (PDF). Holy See. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2013-09-05. Iliwekwa mnamo 2012-10-21.
{{cite journal}}
: Cite journal requires|journal=
(help); Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ Bauman, Michelle (3 Januari 2012 (1 Januari 2012 print edition)). "New U.S. Anglican Ordinariate Has an Ordinary". National Catholic Register. EWTN News, Inc. Iliwekwa mnamo 2012-01-06.
{{cite web}}
: Check date values in:|date=
(help) - ↑ William H. Stetson, "History of the Pastoral Provision"
- ↑ 4.0 4.1 Jack D. Barker, "A History of the Pastoral Provision for Roman Catholics in the USA", chapter 1 of Stephen E. Cavanaugh, Anglicans and the Roman Catholic Church (Ignatius Press 2011 ISBN 9781586174996)
- ↑ Office of the Ecclesiastical Delegate for the Pastoral Provision
- ↑ "Jerry Fiteau, "New ordinariate and 1980 pastoral provision: An analysis"". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-02-10. Iliwekwa mnamo 2012-10-21.
- ↑ "2012 Anglican Use Conference". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2012-10-21.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2005-07-09. Iliwekwa mnamo 2012-10-21.
Viungo vya nje
hariri- Letter of the Congregation for the Doctrine of the Faith communicating the pastoral provision Ilihifadhiwa 4 Juni 2004 kwenye Wayback Machine.
- Office of the Ecclesiastical Delegate for the Pastoral Provision Ilihifadhiwa 21 Machi 2012 kwenye Wayback Machine.
- Parishes Ilihifadhiwa 6 Agosti 2012 kwenye Wayback Machine.
- Anglican Use Society Ilihifadhiwa 9 Julai 2005 kwenye Wayback Machine.
- Unitatis Redintegratio, Decree from Second Vatican Council
- A Place Has Been Prepared: "Anglican Use" Catholic Parishes (article) Ilihifadhiwa 24 Desemba 2013 kwenye Wayback Machine.
- Historical documents on Anglican-Roman Catholic relations
Liturujia
hariri- The Book of Divine Worship (BDW) Ilihifadhiwa 20 Februari 2009 kwenye Wayback Machine.
- Online version of Anglican Use Mass, Rite 1, according to the BDW Ilihifadhiwa 16 Septemba 2000 kwenye Wayback Machine.
- Online version of the Daily Office from the BDW
- Text of the Anglican Use Mass
Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Liturujia ya Canterbury kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |