Louvre ni jumba la maonyesho la mjini Paris, Ufaransa, ambalo linavutia mamilioni ya wageni wanaozuru hapo kwa sababu ya mkusanyiko wa sanaa zilizojaa katika jumba hilo. Kiasili ilikuwa jumba la wafalme wa Ufaransa katika mji wa Paris. Tangu uhamisho wa mfalme Louis XIV aliyejenga jumba mpya huko Versailles ilikaa tu ikatumiwa kwa shughuli mablimbali kati yao kupokea kazi za sanaa. Tangu mapinduzi ya Ufaransa ilifunguliwa kwa watu wote. Maonyesho ya sanaa yaliendeleakupanushwa na kuboreshwa leo hii Louvre ni makumbusho na maonyesho ya sanaa duniani inayotembelewa na watu wengi kila mwaka.

Makumbusho ya Louvre

Picha iliyomaarufu kabisa katika jengo la Louvre ni ile ya Mona Lisa iliyochorwa na Leonardo da Vinci, lakini pia kuna michoro ya wasanii wengine kama vile Renoir, Rembrandt, Rubens, na Titian. Piramidi mpya katika uwanja wa jumbaa ilijengwa na I. M. Pei.

Pia kuna sanamu za kuchonga katika jengo hilo la Louvre. Masanamu yaliyomaarufu katika jengo hilo ni pamoja na la Venus de Milo na Nike wa Samotraki.

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Louvre kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES