Michezo ya Olimpiki ni mashindano makubwa ya michezo mbalimbali duniani inayofanyika kila baada ya miaka minne.

Michezo ya Olimpiki

Bendera ya Olimpiki yaonyesha pete tano

Michezo ya Olimpiki imekuwa na historia ndefu katika vipindi viwili:

Michezo hii ya kisasa imeendelea kila baada ya miaka minne isipokuwa 1916, 1940 na 1944 kwa sababu ya Vita Kuu ya Kwanza na ya Pili ya Dunia.

Michezo ya kisasa hufanyika katika mji tofauti kila safari. Michezo ya 2004 ilifanyika Athens, ya 2008 huko Beijing na ya 2012 London.

Kuna tofauti kati ya michezo ya kiangazi na michezo ya majira ya baridi.

Washindi watatu wa kwanza wa kila mashindano hupewa medali ya dhahabu, fedha au shaba.

Pete olimpiki

Pete tano za Olimpiki ni alama na nembo ya michezo tangu mwaka 1913. Pete tano zenye rangi tofauti humaanisha mabara matano. Zote zinashikamana kumaanisha ushirikiano wa kimataifa.

Viungo vya Nje

  Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Michezo ya Olimpiki kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES
Done 1