Milima ya Skandinavia

Milima ya Skandinavia (kwa Kiingereza: Scandinavian Mountains) ni safu ya milima ambayo hupitia kwenye Rasi ya Skandinavia.

Mahali pa milima ya Skandinavia kwenye ramani

Pande za magharibi za milima hiyo huteremka vikali kwenye Bahari ya Kaskazini na Bahari ya Norwei, ambapo huunda fyord za Norwei.

Upande wa kaskazini inaunda mpaka kati ya Norwei na Uswidi, ikiendelea katika Mzingo aktiki. Sehemu ndogo ya masafa huingia Ufini, ambako si marefu tena.

Mlima wa juu zaidi katika safu hiyo ni Galdhøpiggen ulioko kusini mwa Norway ukiwa na mita 2469 juu ya usawa wa bahari. Mlima mkubwa upande wa Uswisi ni Kebnekaise ukiwa na mita 2104 juu ya UB. Halti ni kilele cha juu zaidi nchini Ufini kwa mita 1324.

Mahali pa safu hiyo karibu na Bahari ya Aktiki na Atlantiki ya Kaskazini pamesababisha kuwepo kwa viwanja vingi vya barafu na barafuto .

Marejeo

hariri
  NODES