Mkesha
Mkesha-milima (Turdus abyssinicus)
Mkesha-milima (Turdus abyssinicus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Muscicapoidea (Ndege kama shore)
Familia: Turdidae (Ndege walio na mnasaba na mikesha)
Ngazi za chini

Jenasi 24:

Mikesha ni ndege wa familia ya Turdidae ambao ni wadogo na wanono. Spishi za jenasi Neocossyphus na Stizorhina zinaitwa shesiafu pia. Rangi yao kuu ni rangi ya kahawia na madoa meupe na meusi; wengine wana rangi ya machungwa au nyekundu na wengine ni weusi. Hula wadudu hasa lakini wanaweza kula wanyama wadogo wengine, kama koa na nyungunyungu, na hata beri. Wengi wanaweza kuimba vizuri sana. Hujenga tago lao kwa umbo wa kikombe na pengine hulawekea matope kwa ndani. Jike huyataga mayai 2-5 yenye vidoa.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri
  NODES
Idea 1
idea 1
iOS 1
mac 7
os 13