Mtume Filipo
Filipo (kwa Kigiriki Φίλιππος, Philippos) ni jina la mfuasi wa Yesu Kristo anayeshika nafasi ya tano katika orodha zote nne za Mitume wa Yesu katika Agano Jipya.
Mitume wa Yesu |
---|
|
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu na Kanisa Katoliki na madhehebu mengine yote ya Ukristo yanayokubali heshima hiyo, lakini kwa tarehe tofauti. Kwa Wakatoliki ni tarehe 3 Mei[1]
Maisha
haririHabari zake zinapatikana hasa katika Injili na Matendo ya Mitume.
Mtu wa Bethsaida, kama Mtume Petro, alikuwa mfuasi wa Yohane Mbatizaji alipoitwa na Yesu amfuate.
Ndiye aliyemletea rafiki yake Natanaeli wa Kana (Injili ya Yohane 1:43-46).
Baadaye aliulizwa na Kristo bei ya mikate inayohitajiwa na umati kabla hajawazidishia ile michache iliyokuwepo (Yoh 6:5-7}.
Pia alimletea Yesu Wagiriki ambao walifika Yerusalemu kwa ajili ya Pasaka wakataka kumfahamu (Yoh 12:20-22).
Hatimaye, katika karamu ya mwisho ya Yesu na mitume wake alimuomba awaonyeshe Baba (Yoh 14:8) akalaumiwa naye kwa kutomtambua ndani yake (Yoh. 14:9).
Eusebi wa Kaisarea, katika Historia ecclesiastica, iii.39, aliripoti maneno ya Papias, askofu wa Hierapoli kwamba Filipo alikuwa na mke na watoto na kwamba alifia dini Hierapolis (mwaka 80 hivi).
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
Marejeo
hariri- Thenashara, Mitume Kumi na Wawili – tafsiri ya P. A. Bunju – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Ndanda 1984 – ISBN 9976-63-030-1
Viungo vya nje
hariri- St. Philip the Apostle article from The Catholic Encyclopedia (1911)
- Catholic Encyclopedia: Apostle article regarding the title "Apostle" from The Catholic Encyclopedia
- Catholic Forum: St. Philip Ilihifadhiwa 26 Februari 2007 kwenye Wayback Machine.
- Holy, All-Praised Apostle Philip Orthodox icon and synaxarion
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtume Filipo kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |