Renaissance
Renaissance (pia: zama za mwamko, mwamko-sanaa, renesansi) ni kipindi cha historia ya Ulaya kilichoanza kunako miaka ya 1400, mwishoni mwa kipindi cha Zama za Kati (ambacho kinajulikana pia kwa jina la Kiingereza Middle Ages), hadi miaka ya 1500, mwanzoni mwa nyakati zetu.
"Renaissance" ni neno la Kifaransa lenye maana ya "kuzaliwa upya". Sababu zilizopelekea kipindi hicho kuitwa hivyo ni kwamba, wakati huo, watu walianza kuwa na shauku ya kujifunza kuhusu mambo ya kale, kwa namna moja au nyingi walijifunza hasa mambo ya Ugiriki ya Kale na Roma ya Kale.
Renaissance ilionekana kama "kuzaliwa upya" kwa masomo hayo. Renaissance mara nyingi ilisemwa kama ndiyo mwanzo wa "modern age".
Wakati huo wa Renaissance, kulikuwa na wasanii wengi sana, wengi wao walikuwa waandishi na wengi wao walikuwa wanafalsafa. Watu walijifunza mambo ya hisabati na sayansi mbalimbali. Mtu aliye mjanja wa kujua vitu vingi huitwa "Mtu wa Renaissance". Leonardo da Vinci, ambaye alikuwa mchoraji, mwanasayansi, mwanamuziki na pia mwanafalsafa, ndiye Mwana Renaissance mashuhurizaidi .
Awali Renaissance ilianzia nchini Italia, lakini punde ikaenea katika Ulaya nzima. Katika Italia kipindi hicho kimegawanyika katika hatua tatu:
- Renaissance ya Awali.
- Renaissance ya Juu
- Renaissance ya Mwisho ambayo pia huitwa kipindi cha Mannerist.
Kipindi kilichofuata baada ya Mannerist kilikuwa kinaitwa Baroko ambacho pia kilienea Ulaya nzima kunako 1600. Nje ya Italia, ni vigumu kuelezea wapi kipindi cha Renaissance kiliishia na wapi kipindi cha Baroko kilianza.
Viungo vya nje
hariri- Links for Middle School students Ilihifadhiwa 10 Juni 2008 kwenye Wayback Machine. from the Courtenay Middle School Library Collection
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Renaissance kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |