Namba tasa ni namba asilia isiyogawiwa kwa namba nyingine isipokuwa kwa 1 na kwa namba yenyewe. Kwa Kiingereza zaitwa "prime numbers".

Mfano:

  • 3 ni namba tasa kwa sababu inagawiwa kwa 1 na kwa 3 lakini hakuna namba nyingine inayoweza kuigawa.
  • 4 si namba tasa kwa sababu inagawiwa kwa 1 na kwa 4 lakini pia kwa 2.

Idadi ya namba tasa haina mwisho na thelathini za kwanza ni 2, 3, 5, 7, 11, 13, 17, 19, 23, 29, 31, 37, 41, 43, 47, 53, 59, 61, 67, 71, 73, 79, 83, 89, 97, 101, 103, 107, 109, 113.

1 haihesabiwi kama namba tasa kwa sababu inagawiwa kwa 1 tu hakuna namba ya pili. 0 si namba tasa kwa sababu hairuhusiwi kugawa kwa 0.

Namba zote nyingine zisizo namba tasa huitwa namba kivunge na zinaweza kupatikana kwa kuzidisha namba asilia mbili.

Kichujio cha Erastothenes.

Kichujio cha Eratosthenes

Mbinu nyepesi ya kugundua namba tasa ndogo ni Kichujio cha Eratosthenes. Ilibuniwa na mwanahisabati na mwanafalsafa Eratosthenes aliyeishi zamani za Ugiriki ya Kale.

  • andika namba asilia zote kwenye karatasi kuanzia 2 hadi namba unayotaka kuifanyia utafiti kama ni namba tasa au la. Usiandike 1 kwa sababu iliyotajwa juu.
  1. anza kwa 2.
  2. futa vizidisho vyote vya namba tasa unazozijua au kuzigundua.
  3. anza na 2 na vizidisho vyake kama 4,6,8,10 na kadhalika.
  4. endelea kwa kufuta 3 (namba tasa inayofuata) na vizidisho vyake kama 6,9,12 na kadhalika.
  5. sasa unarudia kuangalia chanzo cha orodha. Namba inayofuata isiyofutwa ni namba tasa tena. Katika mfano huu utakuwa ni 5. Endelea kufuta vizidisho vyake.
  6. Kwa njia hii unarudia kuangalia orodha upya na kugundua namba tasa zote zilizomo.

Matumizi

Kuna matumizi ya namba tasa katika maisha ya kila siku kwenye namba za siri za kadi za benki au kadi za simu pia kwenye simu za mkononi. Nuymba ya namba ya siri mara nyingi ni zidisho la namba tasa mbili kubwa. Ni rahisi kuzidisha namba tasa mbili lakini ni kazi kubwa mno kugundua zao ilikuwa tokeo la namba zipi.

  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Namba tasa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES