Nelson Mandela Square
Nelson Mandela Square ni kituo cha manunuzi kilichopo huko Sandton, Johannesburg, Afrika Kusini. Kinajumuisha eneo kubwa la wazi lililojengwa kwa mtindo wa kufanana na kituo cha mji wa kitamaduni cha Ulaya, na eneo la ofisi. Kituo hicho hapo awali kilijulikana kama Sandton Square ambapo baadaye kilikuja kupewa jina la rais wa zamani wa Afrika Kusini na mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi Nelson Mandela mnamo Machi 2004. Sanamu ya Mandela yenye urefu wa mita sita ilizinduliwa katika hafla ya kubadilisha jina la uwanja huo. [1] [2] Kituo hicho kimeunganishwa na kituo kikubwa cha manunuzi cha Sandton City, ambapo vyote kwa pamoja vinaunda moja ya majengo makubwa ya rejareja barani Afrika huku vituo hivyo vikiwa na maduka zaidi ya 400. Jengo la Michelangelo Towers pia linapakana jirani na kituo-mraba cha Nelson Mandela Square. [3]
Historia
haririKituo-Mraba hicho, ambacho wakati huo kilijulikana kwa jina lake la asili la Sandton Square, kilifunguliwa kwa umma mnamo 1994. Kituo cha ununuzi kiliundwa kwa mtindo wa faux-Italian na kituo-mraba hicho kiliundwa ili kufanana na kituo-mraba cha St Marks Square kilichopo huko Venice . [4] Muundo wake ulijumuisha maktaba, ukumbi wa michezo na nyumba ya sanaa. [4]
Katika kuadhimisha miaka 10, mwaka 2004, kilipewa jina rasmi la Nelson Mandela Square baada ya kuzinduliwa kwa sanamu ya Mandela yenye urefu wa mita sita. Ilikuwa ni sanamu ya kwanza ya umma ya Mandela nchini humo. Ilizinduliwa Julai 2002 na kukamilishwa Februari 2004 na Wachongaji wa Afrika Kusini Kobus Hattingh na Jacob Maponyane. Ina uzito wa takriban tani 2.5.
Uamuzi wa kubadili jina la Kituo-mraba hicho baada ya Mandela kukosolewa na baadhi ya watu kwa vile Mandela alikuwa amesimama kwa muda mrefu kuwatetea watu wasiojiweza na viwanja hivyo katika eneo lenye utajiri mkubwa wa mali nchini humo. Gary Vipond, meneja wa Kituo-mraba hicho, alitetea uamuzi huo kwa kueleza kuwa, "Kituo-mraba hiki kina matumaini, kinajieleza na kinajiamini, kama Madiba jive, na kinawakilisha hadithi ya mafanikio ya kisasa, ya kimfumo na ya ulimwengu." [5]
Kituo hicho cha manunuzi kimeunganishwa na Jiji la Sandton na, kwa pamoja, vinaunda eneo kubwa zaidi la rejareja barani Afrika .Kituo-mraba chenyewe kina eneo lenye takriban mita za mraba 1000 na kina maduka mengi, migahawa na maktaba kwenye moja ya mwisho wake wa mbali.
Marejeo
hariri- ↑ "Eish!". www.southafrica.net.
- ↑ http://www.southafrica.info/mandela/mandela-statue.htm
- ↑ "Michelangelo Hotel : Nelson Mandela Square". nelsonmandelasquare.co.za. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-05-22. Iliwekwa mnamo 2024-10-07.
- ↑ 4.0 4.1 "Nelson Mandela Square".
- ↑ Chandrea Gerber. "Joburg unveils Mandela statue". South Africa Info - Joburg unveils Mandela statue. South Africa Info. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Aprili 2015. Iliwekwa mnamo 12 Aprili 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Nelson Mandela Square kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |