Shesiafu

(Elekezwa kutoka Neocossyphus)
Shesiafu
Shesiafu mwekundu (Stizorhina fraseri)
Shesiafu mwekundu (Stizorhina fraseri)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Passeriformes (Ndege kama shomoro)
Familia ya juu: Muscicapoidea (Nedege kama shore)
Familia: Turdidae (Ndege walio na mnasaba na mikesha)
Ngazi za chini

Jenasi 2:

Shesiafu ni ndege wa jenasi Neocossyphus na Stizorhina katika familia ya Turdidae. Ndege hawa ni aina ya mikesha na waitwa pengine jina hili. Wanatokea Afrika tu. Rangi yao kuu ni rangi ya kahawia na kwa kawaida tumbo lao ni jekundu au kahawiachekundu. Hula wadudu hasa lakini wanyama wadogo wengine pia. Mara kwa mara huungana na ndege walawadudu wengine karibu na safu za siafu wakikamata wadudu na wanyama wadogo ambao wanawakimbia siafu. Lakini spishi za Stizorhina hukamata wadudu mara nyingi zaidi kama shore (kwa hivyo jina la kiingereza “Flycatcher-thrush”). Hujenga tago lao kwa umbo wa kikombe mtini. Jike huyataga mayai 2-4.

Spishi

hariri
  NODES
Idea 1
idea 1
os 5