Neptuni (kisasili)

(Elekezwa kutoka Neptunus)

Kwa matumizi tofauti ya jina hili angalia Neptun na Neptuni (elementi)

Mosaiki ya Neptunus, Palermo, Italia).

Neptunus alisadikiwa na watu wa Roma ya Kale kuwa mungu mmojawapo (kwa Kilatini "Neptunus": ni sawa na mungu wa Ugiriki wa kale "Poseidon") aliyetawala bahari na mito.

Lugha nyingi duniani zimetumia jina hilo kwa ajili ya sayari ya nane kutoka jua, kwa sababu katika tamaduni mbalimbali astronomia ya zamani haikujua sayari hiyo iliyojulikana tangu kupatikana kwa darubini tu, hivyo hazikuwa na jina kwa ajili yake. Kwa Kiswahili, sayari hiyo wakati mwingine inaitwa Kausi lakini hapa wikipedia tunatumia jina la kimataifa Neptun.

  NODES
os 3