Nguzo tano za Uislamu

(Elekezwa kutoka Nguzo Tano za Kiislamu)

Nguzo tano za Uislamu (kwa Kiarabu: أركان الإسلام arkan al-islam, pia أركان الدين arkan ad-din yaani nguzo za dini) ni ibada au matendo yanayoaminiwa kuwa ya kimsingi katika Uislamu. Zimepata hadhi maalumu kwa sababu zinatajwa katika "hadith ya Jibril". Kwenye masimulizi ya hadith ile malaika Jibril alimwuliza Mtume Muhammad "Uislamu ni nini?" na huyu alijibu kwa kutaja matendo matano yafuatayo.

Nguzo tano za Uislamu.
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya

Uislamu

Imani na ibada zake

Umoja wa Mungu
Manabii
Misahafu
Malaika
Uteule
Kiyama
Nguzo za Kiislamu
ShahadaSwalaSaumu
HijaZaka

Waislamu muhimu

Muhammad

Abu BakrAli
Ukoo wa Muhammad
Maswahaba wa Muhammad
Mitume na Manabii katika Uislamu

Maandiko na Sheria

Qur'anSunnahHadithi
Wasifu wa Muhammad
Sharia
Elimu ya Sheria za KiislamuKalam

Historia ya Uislamu

Historia
SunniShi'aKharijiyaRashidunUkhalifaMaimamu

Tamaduni za Kiislamu

ShuleMadrasa
TauhidiFalsafaMaadili
Sayansi
SanaaUjenziMiji
KalendaSikukuu
Wanawake
ViongoziSiasa
Uchumi
UmmaItikadi mpyaSufii

Tazama pia

Uislamu na dini nyingine
Hofu ya Uislamu

Kwa kawaida hizi nguzo tano zinafundishwa katika madhehebu ya Wasunni jinsi inavyoonyeshwa hapo chini.

Washia hawahesabu shahada kati ya nguzo tano wakiona shahada pamoja na imani ya Kiislamu ni msingi wa nguzo tano, halafu wanaongeza "wilayat" yaani kukubali uongozi wa Maimamu kama nguzo ya tano.

  1. Shahada: (Kiarabu: الشهادة) Nguzo ya kwanza katika Uislamu ni ungamo la imani ambalo hujumuisha kutamka kauli mbili: Hakuna mungu ila Allah, na Muhammad ni Mtume wake. Ni kawaida kutamka kauli kwa lugha ya Kiarabu "lā ʾilāha ʾillā-llāh muḥammadun rasūlu-llāh (لَا إِلٰهَ إِلَّا الله مُحَمَّدٌ رَسُولُ الله) ". Kauli hizo hutolewa pale mwanadamu anapoingia Uislamu. Hurudiwa kila siku mara tano wakati wa sala.
  2. Salat: (Kiarabu: صلاة‎) ni sala inayofuata utaratibu maalumu mara tano kila siku: Asubuhi, mchana, alasiri, jioni na usiku. Kabla ya kuingia katika ibada hii Mwislamu anapaswa kufanya wudhu ambayo ni tendo la kutakasa mwili kwa maji au -kama hakuna- kwa kutumia vumbi badala yake. Salat ina maneno yake na pia namna ya kusimama au kujinama. Salat hii ni tofauti na dua (دعاء) au sala ya kuomba kwa hiari.
  3. Zakat: (Kiarabu: زكاة‎‎) Nguzo ya tatu ya Uislamu nayo ni ibada inayomuelekeza Mwislamu kuwaangalia Waislamu wenzake kwa hali na mali, na kushughulikia mahitaji yao ya maisha, kwa kutoa fungu la mali yake asilimia 2.5 kila mwaka kwa mwenye uwezo na kuwapa wale walio maskini na wasiojiweza ili nao waweze kuishi vizuri.
  4. Funga/Saumu: (Kiarabu: صوم) Wakati wa mwezi Ramadani kila Mwislamu anapaswa kufunga chakula na kinywaji chote kuanzia asubuhi hadi jioni. Watoto na wagonjwa hawapaswi kutekeleza wajibu huu. Waislamu wanaona maana ya ibada hii kumkurubisha Mwislamu na Mola wake na kumfanya amche na kumuogopa zaidi, kwani saumu humsaidia Mwislamu kufahamu shida na taabu ambazo wale wasiokuwa na uwezo wanazipata wakiwa na njaa na hawana cha kukila, na kwa hivyo, huingiwa na huruma na kuwa na moyo wa kutaka kuwasaidia na kuwaondoshea shida hizo.
  5. Hajj (Kiarabu: الحجّ alhajj): Kila Mwislamu mwenye uwezo anatakiwa kwenda hijja Maka mara moja katika maisha yake wakati wa mwezi Dhul-Hija. Nguzo hii inawapa fursa Waislamu ulimwenguni kukutana na wenzao na kujua hali zao na kupata nafasi ya kuomba maghfira na msamaha kwa madhambi yao katika mkutano mkubwa kabisa wa wanadamu ulimwenguni.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES