Pemba ni kisiwa kilichopo takriban 50 km kaskazini ya Unguja katika Bahari Hindi. Visiwa vyote viwili ni sehemu za Jamhuri ya Watu wa Zanzibar katika Tanzania. Umbali na Tanganyika au Tanzania bara ni 50 km.

Ramani ya Kisiwa cha Pemba
Visiwa vya Zanzibar (Unguja na Pemba)
Makala hii inahusu Kisiwa cha Pemba. Jina Pemba linatumika pia kwa ajili ya Pemba katika Msumbiji na Pemba wilaya pamoja na mji huko Zambia.

Pemba pamoja na visiwa vidogo karibu nayo ina wakazi 360,797 katika eneo la 980 km².

Miji muhimu ya Pemba ndiyo Chake Chake, Mkoani na Wete.

Pemba kuna mikoa miwili kati ya mikoa 26 ya Tanzania ambayo ni

Uchumi wa Pemba ni hasa kilimo pamoja na uvuvi. Mazao ya sokoni hulimwa hasa karafuu.

Katika utamaduni wa Pemba kuna desturi ya kipekee katika Afrika ndiyo mchezo wa ng'ombe iliyorithiwa na Wareno walipokuwa na athari kisiwani karne zilizopita.

Viungo vya nje

hariri

Wapicha

hariri



  NODES