Penalti (kutoka Kiingereza penalty) ni istilahi ya lugha ya michezo, hasa mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa pete n.k.

Lothar Matthäus (Ujerumani) akipiga penati katika mchezo dhidi Bulgaria wakati wa Kombe la Dunia 1984

Katika soka

hariri

Katika soka, penalti ni nafasi ya mchezaji mmoja kupiga mpira kwa lango la wapinzani kutoka nukta iliyopo mita 11 mbele ya goli. Hapa hawezi kushambuliwa au kuzuiliwa na mchezaji mwingine.

Nafasi hii inatolewa kama mchezaji wa timu inayotetea goli lake anafanya kosa katika eneo la penalti ambalo ni eneo karibu na goli (kwa mpira wa mguu umbali wa mita 16.5). Penalti mara nyingi inaleta goli, kwa hiyo inaweza kuamulia matokeo ya mchezo. Hapo kupata penalti ni kama adhabu kwa timu iliyotetea goli lake kwa kukosea kanuni za michezo.

Kusudi lake ni kuzuia matumizi ya mbinu zisizo halali katika eneo muhimu karibu na goli.

Kwenye mashindano makubwa ya soka penalti inatumiwa pia kama njia ya kumpata mshindi kama mchezo unaishia sare (droo). Hapa kila timu inapewa nafasi 5 za kupiga mpira kutoka nukta ya penalti yaani kwa umbali wa mita 11. Kama tokeo ni sare tena yote hurudiwa hadi timu moja iko mbele na hivyo kuwa mshindi.

  Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Penalti kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES