Rashid Bin Saeed Al Maktoum
Kigezo:Infobox prime minister Sheikh Rashid Bin Saeed Al Maktoum (1912 - 7 Oktoba 1990) (Kiarabu: راشد بن سعيد آل مكتوم) alikuwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu na Emir (mtawala) wa Dubai. Yeye alitawala kwa miaka 32, mpaka kifo chake.
Sheikh Rashid Bin Saeed Al Maktoum anaweza kuitwa aliyekuwa na maona ya UAE ya kisasa Ilikuwa wakati wa utawala wake ambapo Dubai ilikua kutoka mji mdogo wa kibiashara hadi mji mkuu wa mkusanyiko. Kufuatia uvumbuzi wa mafuta katika kanda hiyo katika miaka ya 1960, moja ya majukumu yake ya kwanza ilikuwa ni ya ujenzi wa bandari ya kisasa na viwanja vya ndege Dubai. UAE ilishuhudia shughuli nyingi za ujenzi katika miaka ya 1970 na nyingi zilikuwa zikifanyika Dubai. Ujenzi wa bandari ya pili katika Jebel Ali, Dubai Dry Dock, Shindaga Tunnel na Dubai Trade Center kwa kutaja wachache. Miradi hizi zimefungua njia ya maendeleo ya baadaye ya mji ambayo yanaendelea mpaka leo. Bintiye aliolewa na kisha Emir wa Qatar ambaye alisaidia katika kugharimia miradi zingine. Emir wa Kuwait alisaidia katika ufadhili wa uchimbaji wa Creek, ambayo ilisababisha Dubai ifanikiwe kama bandari ya kuingia UAE. Mama yake Sheikha Hussah bint Murr alimiliki ardhi, alihusika katika biashara na aligawana uongozi wa Dubai.
Sheikh Rashid alikuwa na wana wanne:
- Maktoum bin Rashid Al Maktoum (1943-2006)
- Hamdan Bin Rashid Al Maktoum (b. 1945)
- Mohammed bin Rashid Al Maktoum (b. 1949)
- Ahmed bin Rashid Al Maktoum (b. 1950)
Aliyemtangulia (kama Waziri Mkuu) na mrithi wake alikuwa mwana wake, Sheikh Maktoum bin Rashid Al Maktoum, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa United Arab Emirates 1971-1979 na ambaye alikuwa Emir ya Dubai kuanzia 7 Oktoba 1990 hadi kifo chake tarehe 4 Januari 2006. Mwanake mwengine, Mohammed bin Rashid Al Maktoum, alichukua nyadhifa hizi zote baada ya kifo cha Sheikh Maktoum.
Mmoja wa viongozi wenye mafanikio zaidi katika Mashariki ya Kati, Sheikh Rashid aliwajibika kwa ajili ya mageuzi ya Dubai katika mji wa bandari ya kisasa na kibiashara. Laini yake maarufu, "babu yangu aliendesha ngamia, baba yangu aliendesha ngamia, mimi naendesha Mercedes, mwanangu aendesha Land Rover, mwanake ataendesha Land Rover, lakini mwanake ataendesha ngamia." Huangazia wasiwasi wake kwamba mafuta ya Dubai yataisha katika muongo mmoja au mbili. Hivyo alifanya kazi ili kujenga uchumi katika Dubai ambao unaweza kuishi baada ya mafuta ya Dubai kuisha.
Marejeo
haririViungo vya nje
haririAlitanguliwa na Sheikh Said II ibn Maktum |
Emir of Dubai 1958—1990 |
Akafuatiwa na Maktoum bin Rashid Al Maktoum |
Alitanguliwa na Maktoum bin Rashid Al Maktoum |
Prime Minister of the United Arab Emirates 1979—1990 |
Akafuatiwa na Maktoum bin Rashid Al Maktoum |
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Rashid Bin Saeed Al Maktoum kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |