Rasi ya Skandinavia

Rasi ya Skandinavia ni rasi kubwa kaskazini mwa Ulaya. Inazungukwa na Bahari Atlantiki upande wa magharibi na kaskazini, halafu na Bahari ya Baltiki upande wa kusini na mashariki. Inaunganishwa na Ulaya bara upande wa kaskazini-mashariki takriban pale ambako mpaka wa Uswidi na Ufini unapatikana. Kwa kusini inatenganishwa na Denmark kwa milango ya bahari ya Kattegat na Skagerak.

Rasi ya Skandinavia (pamoja na Ufini huitwa "Fennoscandia" kwa Kiingereza).

Ndani ya rasi ya Skandinavia kuna nchi za Uswidi na Norwei.

Jina la rasi linatokana na "Skandinavia" ambalo ni jina la kujumlisha nchi za Norwei, Uswidi, Denmark na Iceland ambazo zote ziko karibu kihistoria na kiutamaduni. Asili ya jina Skandinavia ni eneo la Skania kusini mwa Uswidi.

Rasi hii ni rasi kubwa ya Ulaya. Ina urefu wa kilomita 1,850 na upana ulio kati ya kilomita 370–805.

Milima mirefu iko Norwei inayofikia kimo cha mita 2,470 juu ya UB. Hapa kuna pia barafuto kubwa za Ulaya.

Hali ya hewa ni baridi kwa jumla; sehemu za kaskazini ziko ndani ya duara ya Aktiki. Katika kusini baridi inapoa na Uswidi kusini hali ya hewa inafaa kwa kilimo. Hata miji mikubwa, kama vile Stockholm na Gothenburg za Uswidi halafu Oslo ya Norwei, iko yote kusini mwa rasi.

Rasilmali ya Skandinvia ni pamoja na ubao kutoka misitu minene, chuma na shaba inayochimbwa katika migodi. Bahari ya Kaskazini mbele ya Norwei ina akiba kubwa za mafuta ya petroli chini ya maji.

  NODES