Rhodos ni kisiwa cha Ugiriki karibu na pwani ya Uturuki.

Rhodos katika Bahari ya Aegean.

Kuna takariban wakazi 120,000. Miji mikubwa ni Rhodos na Lindos.

Historia

hariri

Rhodos ina historia ndefu.

Katika nyakati za kale ilikuwa na Sanamu ya Kolossos iliyohesabiwa kati ya maajabu ya dunia.

Wakati wa vita za misalaba kisiwa kilikuwa kituo muhimu ya wamisalaba wa chama cha hospitali ya Mt. Yohane wa Yerusalemu.

Mwaka 1644 Waosmani walipofaulu kuteka kisiwa na wamisalaba walihamia Malta.

Mwaka 1912 kisiwa kikatwaliwa na Italia kikawa sehemu ya Ugiriki ya kisasa tangu mwaka 1946.

Uchumi wa kisiwa hutegemea hasa utalii.

  Makala hii kuhusu maeneo ya Ugiriki bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rhodos kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES