Shesiafu
Shesiafu | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Shesiafu mwekundu (Stizorhina fraseri)
| ||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 2:
|
Shesiafu ni ndege wa jenasi Neocossyphus na Stizorhina katika familia ya Turdidae. Ndege hawa ni aina ya mikesha na waitwa pengine jina hili. Wanatokea Afrika tu. Rangi yao kuu ni rangi ya kahawia na kwa kawaida tumbo lao ni jekundu au kahawiachekundu. Hula wadudu hasa lakini wanyama wadogo wengine pia. Mara kwa mara huungana na ndege walawadudu wengine karibu na safu za siafu wakikamata wadudu na wanyama wadogo ambao wanawakimbia siafu. Lakini spishi za Stizorhina hukamata wadudu mara nyingi zaidi kama shore (kwa hivyo jina la kiingereza “Flycatcher-thrush”). Hujenga tago lao kwa umbo wa kikombe mtini. Jike huyataga mayai 2-4.
Spishi
hariri- Neocossyphus rufus, Shesiafu Mkia-mwekundu (Red-tailed Rufous Thrush au Ant-thrush)
- Neocossyphus poensis, Shesiafu Mkia-mweupe (White-tailed Rufous Thrush au Ant-thrush)
- Stizorhina finschi, Shesiafu wa Finsch (Finsch's Rufous Thrush au Finsch's Flycatcher-thrush]])
- Stizorhina fraseri, Shesiafu Mwekundu (Fraser's Rufous Thrush au Rufous Flycatcher-thrush)