Tauni (au kipukusa; kwa Kiingereza: plague au pestilence) ni ugonjwa unaoambukiza watu wengi sana unaosababishwa na bakteria Yersinia pestis ya familia Enterobacteriaceae.

Yersinia pestis iliyokuzwa mara 200 ikiwa na lebo ya fluoro. Bakteria hii ndiyo sababu ya aina mbalimbali za tauni.
Tauni ya majipu inasababisha tezi za limfu zifure.

Inapatikana kwa kawaida katika maeneo kadhaa ya dunia yasiyo na maendeleo.[1]

Kadiri ya athira juu ya mapafu na hali nyingine za mgonjwa, inaweza kuenea kupitia hewa, kwa kugusana na kwa nadra kwa njia ya chakula kisichopikwa vya kutosha.

Dalili zinategemea ugonjwa umemshika mtu wapi zaidi: tezi, mishipa ya damu au mapafu.

Tiba ikiwahi inaweza kumponya mtu.

Historia

hariri

Zamani tauni iliua watu wengi: kwa miaka michache hata nusu ya Wachina wote, halafu theluthi ya Wazungu wote.

Biblia inazungumzia ugonjwa huo.

Barani Afrika ugonjwa ulienea mara kadhaa, lakini mtawanyiko wa watu katika maeneo makubwa haukuisaidia tauni kuwapata watu wengi zaidi kama kwenye msongamano mkubwa.

Ni maarufu juhudi za Wajerumani kukomesha tauni katika koloni lao la Afrika Mashariki ya Kijerumani mwishoni mwa karne ya 19 kwa kulipa kiasi kadhaa kwa kila mzoga wa panya, mnyama anayesambaza bakteria hizo kupitia viroboto wake.[2]

Tanbihi

hariri
  1. "WHO IHR Brief No. 2. Notification and other reporting requirements under the IHR (2005)" (PDF). Iliwekwa mnamo 2014-08-24.
  2. Pugu Hadi Peramiho - kimehaririwa na P. Gerold Rupper, OSB, BPNP, Peramiho 1988, ISBN 9967 67 031 1

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tauni kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  NODES